Monday, August 3, 2009

Somo la 6: Kutembea Nuruni: Kuwakataa Wapinga Kristo

(1 John 2:18-29, 2 Corinthians 1)

1, 2 & 3 Yohana: Somo la 6


Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.



Utangulizi: Wiki iliyopita tulijifunza kuwa watu werevu walikuwa na matazamio ya masuala ya umilele na utajiri wa milele. Kwa nini ni waerevu kufanya hivi? Kwa sababu dunia hii itaishia kuungua wakati ambapo wale walio na mtazamo wa kimbingu watakuwa na uzima wa milele wakifurahia hazina za milele. Mtazao huo hugawanya "walio wa kidunia" kutoka kwa wale waaminio. Wiki hii Yohana anageukia uzingativu wake kwenye tatizo lisilokuwa la kawaida. Anatuonya kuhusu "wapinga Kristo." Hebu tujitose kwenye kwenye ujifunzaji wetu wa Biblia na kubaini kuhusu hawa  wapinga Kristo na jinsi ya kujizuia kutumbukia katika tatizo la upinga Kristo!


 


 

  1. Saa ya Mwisho


     

    1. Soma 1 Yohana 2:18. Hawa "watoto" ni akina nani? (1 Yohana 2:1 ilianza kwa kauli hiyo hiyo, "watoto wangu." Tuliamua hapo kabla kuwa hawa ni wafuasi wa Yesu. Kumbuka kutoka wiki iliyopita kwamba "watoto," kinyume na "akina baba" au "vijana" (Tazama 1 Yohana 2:12-14), inawarejea waumini wapya. Hawa ni watu ambao wana mengi ya kujifunza.)


       

      1. "Saa ya mwisho." Yohana anamanisha nini katika hili? Saa ya mwisho ya historia ya dunia?


         

      2. Soma Kumbukumbu la Torati 18:20-22. Kama Yohana anamaanisha kuwaambia wasomaji wake mwisho wa wakati umekaribia, je, hiyo hufunua kuwa yeye ni nabii wa uongo na kwamba tuache mara moja kusoma barua zake?


 

  1. Umesikia "mwisho wa wakati," "zama za mwisho," "siku za mwisho" na kauli kama hizo. "Saa ya mwisho" inaonekana kuwa mwisho wa miisho, sawa?


 

  1. Soma Mathayo 24:30-34. Yesu anasema nini: kwamba wale waliokuwa wakimsikiliza hapo awali watauona ujio wake wa mara ya pili?


     

    1. Kama ndivyo, je, Yohana alikuwa anarudia tu kitu kisicho sahihi ambacho Yesu alikisema?


       

    2. Kwa kuwa hatuwezi kumpigia kura Yesu kama nabii wa uongo, tuupigie kura Ukristo wote?


 

  1. Soma Mathayo 24:1-3? Unafikiria nini juu ya ubora wa swali la faragha la wanafunzi?
    1. Tatizo limeunganishwa? (Ndiyo. Wanafunzi wanauliza kuhusu uharibifu wa hekalu na mwisho wa dunia. Waliamini kimakosa kwamba matukio hayo mawili yalikuwa ni tukio moja.)


       

    2. Yesu anajadili swali lipi? (Uharibifu wa hekalu Yerusalemu. Hili lilitendeka mwaka 70 BK. Kama Yesu bado anaongelea kuhusu ule uharibifu, kauli ya "kizazi hiki" ni ya kweli.


     

    1. Yesu anaonekana kuunganisha Ujio Wake wa Mara ya Pili na uharibifu wa hekalu. Je, huu ni "usaidizi wa upotoshaji," "uongo wenye manufaa" (ili tusikatishwe tamaa), au kuna kitu kingine kinaendelea? Je, kauli ya Yesu ni kitu ambacho kinatusaidia kuelewa "saa ya mwisho" ya Yohana? (Jiweke katika viatu vya wasikilizaji.. Hekalu ndilo lililokuwa kitovu cha kuabudu kuliopo. Mfumo wa kuabudu wa hekalu ulikuwa ni ishara ya kifo cha Yesu, maisha na kutuombea dhambi zetu. Uharibifu wa hekalu muda mfupi baada ya Yesu kusulubiwa ulianzisha ukurasa mpya kwa wafuasi wa Mungu-siku za mwisho, mwisho wa zama, saa ya mwisho.)


       

      1. Je hii inaweza kuwa ni sababu kuwa wanafunzi hawakuweza kufikiri dunia bila ya hekalu? (Ndiyo. Kama mfumo wa ibada kwa Mungu wa ukweli ungetoweka, ingemaanisha Mungu hakuwa tena akiuongoza. Hiyo isingewezekana. Wanafunzi hawakuweza kuelewa bado kuwa Yesu ndiyo alikuwa sababu mfumo wa kafara ukawepo.)



  1. Mpinga kristo


     

    1. Hebu na tuendelee mbele na 1    Yoh 2:18. Ni kwa jinsi gani makristo wa uwongo wanahusika na saa ya mwisho? ( Haya machafuko katika mfumo wa ibada unatoa fursa kwa walimu wa uwongo.)


 

  1. Je ni wapinga kristo wangapi tulio nao? (Inaonekana ni wengi)\
  2. Je unafikiri Yohana anamaanisha nini kwa neon "mpinga kristo" na "wapinga kristo wengi?" (Inaonekana yupo mpinga kristo mkuu. Lakini yaonekana wapo wapinga kristo wengine wadogo pia.)


 

  1.   Mpinga kristo ni neon tete. Hebu tusome 1 Yohana 2:19-22 kupata picha hasa ya nini neon hilo humaanisha.


     

    1. Je wapinga kristo ni watu waliokuwa wazuri awali wkitembea katika nuru? ( Walihusiana na kundi la waaminio. Yohana anasema kuondoka kwao kunaonyesha kuwa hawakuwahi kamwe kuwa sehemu ya kundi. Japo, walionekana kuwa sehemu ya kundi.)


       

    2. Ni njia ipi ya awali kabisa ya kumtambua mpinga kristo? (Yeye asemaye uwongo juu ya kweli. Ukweli wa msingi ukiwa ni kuwa Yesu ni Mungu. Ukikataa ya kwamba Yesu si Bwana, utakuwa unamkataa Mungu baba pia.)


 

  1. Ni kwa jinsi gani hiyo ni ukweli? Ni kwa jinsi gani hatukuweza kuamini katika "Mungu mmoja (kama ilicyo kwa Wayahudi na Waislamu) wa agano la akale bila kukuibaliana na huu wingi wa Mungu ambao wakristo wanautangaza ? (Kama hukufahamu kwambaYesu ndiyo alikuwa sababu kwa mpango wa hekalu wa Mungu wa ondoleo la dhambi, kivyovyote hutoweza kuelewa ukweli ao kuweza kuelezea ukweli juu ya Mungu. Katika mwaka 70 A.D. saa ya mwisho ilifika ambapo watu aidha walielewa mpango wa Mungu na kufanya mabadiliko kutoka huduma za ishara na kumtazama Yesu, au waliachwa nyuma katika ujinga.)


 


 


 

Soma 1Yohana 2:23. Je hii inaleta mantiki kwako? (Kama kukmubali Yesu na kafara yake ni njia mpaaya iliyoainishwa ya kuondokana na dhambi, hivyo itakuwa ndiyo njia pekee ya kumwendea Mtakatifu Mungu Baba.)   


 

  1.  Soma 1Yohana 2:24-25. Nini uhusiano kati ya uzima wa milele na Yesu? (Kwa kuwa kifo cha Yesu kwa niaba yetu (tulikuwa na Yesu pale naye alipofariki) ndiyo ufunguo wa ondoleo letu la dhambi, kifo chake pia ni ufunguo kwa maisha yetu ya umilele!)


 

   
 

  1. Kupakwa mafuta


     

    1. Tumejifunza kwamba ni muhimu kuhifadhi " kile tulichosikia tangu mwanzo" (1 Yoh 2:24). Ni nini kinachofanya ukweli udumu? (soma tena 1 Yohana 2:20: kutawazwa na Mtakatifu.")


     

    1. Mtakatifu iatakuwa inazungumzia Mungu. Kupakwa gani mafuta huku kuliko kwa muhimu?


 

  1. Soma 2 Wakorintho 1:21-22. Fungu hili huelezeaje upakwaji wa mafuta?


 

  1. Tunafahamu jinsi ya kulipia kitu mapema kidogo kwa kiasi (deposit) kwa kitu tutakachonunua. Ni kwa jinsi gani roho mtakatifu ni deposit kwa ujio wa Yesu mara ya pili? Ni kwa jinsi gani roho mtakatifu ni deposit inayotufanya tuendelee kuamini katika Yesu? (Deposit ni sehemu ya bei ya ununuzi. Ni sampuli ya baki. Tutakapoenda mbinguni wakati wa ujio wa Yesu mara ya pili tutaishi katika uwepo wa Mungu. Tunaweza kuanza kuelewa sasa hivi ni kwa vipi tutaishi mbele ya uwepo wa Mungu wakati tukiwa tumejawana roho mtakatifu.)


     

  1. Hofu yako kubwa ni ipi katika kumwamini kwako Mungu?( kwamba tunaamini kitu ambacho siyo kweli. Kwa kawaida huwa nasoma vitabu maarufu vya kisayansi na jambo kubwa mara nyingi ni kuwa hakuna Mungu, ila palitokea uibikaji (evolution))

    1. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu anatupa uthibitisho wa uwepo wa Mungu? (Kama unajua Roho Mtakatifu anafanya kazi katika maisha yako basi unauthibitisho ya kuwa Mungu yupo na kwamba Biblia ni ya kweli.)


 

  1. Soma Yohana 16:13. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu aweza kutuongoza katika kuujua ukweli kuhusu Mungu? (Mara nyingine huwa nashangaa sana ni kwa jinsi gani hawa wanasayansi wanaweza kuwa wapumbavu. Wanaandika vitabu juu ya kanunni zinazosimamia mfumo wa uumbaji. Wanaafiki ya kwamba wanfahamu kanuni nyingi kupitia vipimo –hawafahamu mantiki ama sababu zinazozunguka kanuni. Wakati katika ulimwengu huu wenye kujali usahihi, kanuni wanaaamini ya kwamba kila kitu kilitokea kwa bahati! Roho mtakatifu anatupa fikra safi na thabiti ya upungufu katika kfumo huo wa fikra.)


 

  1. Soma 1 Yohana 2:-26-27. Je hii humaanisha kwamba hunihitaji mimi? Huhitaji mwongozo wa kujifunza Biblia? Hatuhitaji nyaraka za Yohana? (Nafikiri Yohana anasema kuwa hatuhitaji walimu wa uwongo. Kama ambavyo unaweza ukawa umeshabaini, jinsi navyoandaa masomo haya ni katika mtindo ambao utakufanya usome Biblia, na kasha kukuuliza maswali juu ya kile ulichokisoma. Lengo langu ni kukusaidia ufikiri juu ya neon la Mungu na kumwacha Roho wa Bwana akuongoze.)
     

  2. Soma 1 Yohana 2:28-29. Wajib u wetu ni upi? (kuendelea kutembea katika nuru!)


 

  1. Rafiki, kama unaamini ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, kama unaikubali kafara yake kwa niaba yako, basi upo katiaka njia ya kuelekea ufalme wa milele. Kama unahitaji msaada (na unauhitaji) je utamwomba roho mtakatifu akujaze?\je utaanza kupata uzoefu sasa wa kuishi mbele za Bwana? Kwa nini usiliombee hilo sasa?


 

  1. Juma lijalo: Kuishi kama watoto wa Mungu


     


     

No comments:

Post a Comment