Monday, August 17, 2009

SOMO LA NANE : KUWAPENDA NDUGU NA DADA

Kuwapenda Ndugu na Dada

(1 John 3:11-24)

1, 2 & 3 Yohana: Somo la 8

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk. Mwombe Roho Mtakatifu aongoze mawazo yako.

Utangulizi: Juma hili sote tutafakari kama wanasheria wa “common law”. Walianzisha wazo kwamba sheria haikutokana na vifungu bali vifungu vilitokana na maamuzi ya mashauri yaliyopita. Hapa tunamaanisha vifungu vya sheria, yaani legislations. Katika muktadha ya awali, unatumia kifungu Sahihi cha sheria endapo tu uliuliza swala/swali Sahihi, wakati katika muktadha ya pili unaoanisha maamuzi ya mashitaka/mashauri yaliyopita na mashitaka yaliyopo ili kupata jibu/kanuni/kifungu Sahihi). Yohana anatupatia “mambo” fulani ili kuweza kutafakari namna ya kuishi tunapokuwa tukiendelea na safari yetu kwenye njia ya kuelekea kwenye mwanga. Hebu tuzame ndani ya somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhuhu kuishi Kibiblia!

I. Kaini Dhidi ya Yesu

A. Juma lililopita tuliishia kwenye somo letu kwa muhtasari wa Yohana wa jinsi tunavyoweza kuwatofautisha watu wema kutoka kwa watu wabaya. Watu wema hufanya vitu vizuri na watu wabaya hufanya mambo mabaya. Hilo lilituacha na swali, “Ni nini, kwa hakika, ni kitu kizuri?” Hebu tuendeleze mjadala wa Yohana kwa kusoma 1 Yohana 3:11. Jiweke kwenye hali ya kwamba nimekupa kanuni moja: “mpendane.” Unaweza kujua namna ya kuishi?

1. Waweza kukabili tatizo kwa kuchukulia upendo (nia/mtazamo) na kuubadilisha kuwa tendo halisi?

2. Miaka kadhaa iliyopita nilitetea Uhuru wa dini wa waumini wa uchawi - wiccans Hilo lilinifundisha kwamba waumini wa dini hiyo wana kanuni moja kuu (the Wiccan Rede) ambayo kimsingi inasema kuwa “Fanya kile unachotaka maadam tu haumdhuru mtu yeyote.” Je, hiyo ni sawa na kuwapenda wengine? (Ningeshukuru kama kila mmoja angefuata kanuni kwamba hawatanidhuru, lakini hitaji la upendo ni matendo zaidi kuliko nadharia).

B. Soma 1 Yohana 3:12. Yohana sasa anatupatia mfano (shauri) kinyume na kanuni. Ni tafsiri gani ya upendo unayoipata kutokana na hili? (Inaonekana kama ile ya Wiccan Rede-Usiue mtu yeyote.)

1. Je, hicho ndio kipimo? Tunawapenda wengine kama tutajizuia/tutaepuka kuwaua?

2. Gundua kwamba Yohana anaandika kuhusu mitazamo/nia za Kaini. Kwa nini Biblia inajadili nia ya Kaini ya kuua? (Badala ya kubainisha kwa hakika nia za Kaini, Yohana anahusianisha matendo yake maovu na mauaji.)

a. Ni matendo gani maovu kwa upande wa Kaini yalileteleza mauaji? (Kutomtii Mungu).

b. Tumeachiwa kutafakari sisi wenyewe mitazamo tarajali. Unafikiri ilikuwa ni ipi? (Wivu dhidi ya Habili na kumwonea wivu Habili kwa kuwa alisimama na Mungu)

c. Kwa nini hilo lilileteleza Mauaji? (Nia za kiovu hupelekea kuwa na matendo maovu ambayo hupelekea mauaji. Wazo ni kwamba dhambi ni endelevu.)

d. Je, kujizuia na mauaji ndicho kipimo cha Yohana cha Upendo? (Hapana. Kwa kuangalia shauri badala ya kanuni, tunaona kwamba mfano wa jambo hasi la Yohana unasheheni katika somo kuhusu nia/mitazamo na asili ya dhambi.)

C. Soma 1 Yohana 3:13. Je, Kaini ni mfano wa jambo hasi kwetu, au ni mfano unaowakilisha dunia? (Kwa kiwango cha chini kabisa, Yohana anatuonyesha kile kisichomaanisha upendo. Siyo mauaji. Anaendelea kusema kuwa mtazamo wa dunia ni chuki, na chuki huleteleza kifo. Unaweza kutarajia dunia kukuchukia.)

1. Hebu tufanye hili kuwa la kawaida. “Wachukiaji” ni neno linalotumiwa na mashoga kuelezea Wakristo wanaoamini kwamba Biblia inazungumzia kuhusu ushoga Bango la kawaida la “mashoga” linasema kuwa “Chuki siyo maadili ya kifamilia.” Je, wana mantiki fulani hapo? Au, ni sehemu ya machukizo ya dunia kwa Wakristo iliyoakisiwa kwao kutuita wachukiaji?

2. Je, Yohana anaandika kuhusu upendo kwa Wakristo wenzetu? (Nadhani.)

a. Je, hilo linafanya suala hili kuwa jepesi? Tunaambiwa kuwapenda wale wanaojiheshimu? (Mahusiano yetu na mashoga yamefanywa kuwa magumu kwa sababu tunasema tabia yao ni ya kidhambi na wao wanaona kuwa ni mambo ya kawaida. Lakini, hata pale tunapojihusisha na Wakristo wenzetu tuna tatizo bado kwa kuwa nao ni wadhambi).

D. Soma 1 Yohana 3:14-15. Yohana anatupatia jaribu gani kujua kwamba tupo kwenye njia sahihi kuelekea nuruni? (Tunawapenda ndugu zetu. Je, tunapiga hatua yoyote hapa? Tumerejea kutafakari kile ambacho “upendo” humaanisha pale tunapojaribu kuubadili kuwa vitendo.)

1. Soma Mathayo 5:21-22. Yesu anasema “hasira=Kitu kama mauaji.” Awali hilo halionekani kuleta mantiki. Je, Yohana anaelezea kauli ya Yesu? (Nadhani hapa Yohana anaendeleza mantiki ileile. Hasira huleteleza chuki ambayo nayo huleteleza mauaji. Usiwe na hasira na kamwe hutaua. Kama ukifanya upendo usimame badala ya/mahali pa hasira basi upo katika njia ya kuelekea nuruni.)

2. Je, tuna viashiria vyovyote vya msingi vya kupima upendo wetu? (Ndiyo. Hasira siyo upendo. Chuki siyo upendo. Mauaji siyo upendo.)

E. Soma 1 Yohana 3:16. Sasa tunapata mfano wa jambo chanya. Upendo ni nini? (Kujitoa maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine.)

1. Je, uko tayari kujitoa maisha yako kwa ajili ya Wakristo wenzako? (Kwa hakika ilikuwa rahisi zaidi pale ambapo tu nilipopaswa kuzuia mauaji!)

2. Je, mjadala wa utoaji mimba unaamuliwa vipi katika muktadha wa hii kanuni ya msingi? (Utoaji mimba ni kuyatoa maisha ya mtu mwingine kwa ajili ya manufaa yetu. Mfano wa Yesu ni kinyume kabisa: kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya mtu mwingine).

3. Utoaji mimba ni wito rahisi wa kimantiki pale unapopimwa na mfano wa Yesu. Ni vipi kuhusu nyanja nyingine za maisha, kama vile muda na fedha. Je, uko tayari kuyaacha haya kwa ajili ya Wakristo wengine?

F. Soma 1 Yohana 3:17. Yohana anasema nini kuhusu upendo na kuwasaidia Wakristo wenzetu walio wahitaji? (Anasema kuwasaidia kunaendana na mantiki ya Yesu kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu.)

1. Kwa nini inaleta mantiki kumsaidia mtu fulani kama Yesu alitupa mfano wa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wengine? (Utatoa nini kwa ajili ya maisha yako? Chochote kile kiwacho, kukitoa si vigumu sana kuliko kuyatoa maisha yako.)

G. Soma 1 Yohana 3:18. Yohana anamaanisha nini pale anaposema kupenda “kwa kweli.” (Hata hivyo kufanya jambo kumsaidia mtu fulani huonyesha kwamba unawapenda. Maongezi yanaweza yasiashirie ukweli wowote kabisa.)

H. Chukulia pale tulipofikia. Mfano mbovu wa Kaini unatuambia tusiue, kuchukia au kukasirika. Kuzuia mauaji na chuki inaonekana kuwa ni rahisi sana . Agano la Kale limejawa na kulaaniwa kwa matajiri wanaopora na kuwadhulumu masikini. Hiyo inaonekana kuleta maana/mantiki. Mjadala wetu hadi sasa ni himaya ya “kanuni ya waumini katika dini za uchawi”. Usiwadhuru wengine. Lakini sasa tunaambiwa kuwa tunatakiwa kutoa vitu vyetu kwa ajili ya Wakristo wahitaji. Kwa nini hili ni gumu sana ? (Tu wabinafsi. Siyo kwamba tu hatutaki kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wengine, hatutaki kutoa vitu vyetu. Tunasema: hebu nao wajishughulishe kutafuta vyao!”.

1. Je, kuna tumaini lolote kwa ajili yetu? (Ndiyo. Hiki ndicho kikubwa kujifunza kuhusu neema, njia (njia ya Yohana ya kuelekea nuruni), na sasa rejea za maamuzi ya mashauri yaliyopita. Kwanza, tumeokolewa kwa neema (1 Yohana 2:1-2). Waliookolewa wapo kwenye njia tofauti na mashauri mabovu ya kaini wakielekea katika shauri jema la yesu.) Tunapaswa kuacha nyuma mauaji, chuki na hasira, na mitazamo yetu iwekwe katika mfano wa Yesu. Mfano wake ndilo lengo letu.)

  1. Matatizo ya Moyo
    1. Soma 1 Yohana 3:19-20. Unadhani Yohana anamaanisha nini pale anapoandika kuhusu dhamira zetu kutushitaki? Je, moyo wako umewahi kukuhukumu? (Hili ndilo jukumu la Shetani na wasaidizi wake-kutushitaki)(Ufunuo 12:10).)
      1. Tunawezaje kutofautisha shutuma za Shetani na uhukumu/uhakiki wa Roho Mtakatifu? (Mungu hutusamehe dhambi zetu tulizozitubu, lakini Shetani anakuwa anaendelea kuzileta mbele yetu ili kutukatisha tamaa. Nafikiri Yohana anasema kuwa kama ukijichunguza matendo yako, na kuona kwamba unapiga hatua mbele kuelekea kwenye mfano wa Yesu wa Upendo, basi unaweza kujiamini kuwa upo kwenye njia yenye nuru. Una “uthibitisho” kuwa maisha yako yanaelekea kwenye uelekeo sahihi.)
    2. Soma 1 Yohana 3:21-22. Kwa nini Yohana tena anarejea habari za kupokea kitu fulani/chochote? Nilidhani tumekubaliana hivi punde tu kwamba tunahitajika kuwapatia vitu wale Wakristo walio wahitaji. (Picha yote sasa imefunuliwa-kama Yesu alikuwa radhi kutupatia maisha/uhai wake, yuko radhi kutupatia vitu. Yohana anafundisha kwamba kama tukiifungua mioyo yetu (na pochi zetu) kwa wale walio wahitaji, Mungu atafungua pochi yake kwetu.)
    3. Soma 1 Yohana 3:23-24. Baada ya huu mjadala kuhusu kuwasaidia wengine, kwa nini Yohana anasema “amri yake” ni “kuliamini jina la Mwana wake?” ( Kama tulivyojadili, Yesu ndiye mfano wa mwisho wa kujitoa kwa ajili ya wengine. Yesu pia ni mfano wa mwisho wa kujitoa kwa ajili ya wengine. Yesu pia ni mfano wa mwisho wa kuheshimiwa kwa ajili ya hili.)
    4. Rafiki, vipi kuhusu wewe? Utadhamiria leo kwamba utawasaidia Wakristo wenzako walio wahitaji? Utagawana nao muda wako na vitu vyako pamoja nao?
  2. Juma Lijalo: Kumwamini Mwana wa Mungu.

No comments:

Post a Comment