Wednesday, June 24, 2009

Lesoni ya 13: Utume

Matendo 1 & 18, 1 Wakorintho 1

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk

Utangulizi: Unamfahamu mtu "mwenye moto" kwa ajili ya Yesu? Je, uliwahi kuwa hivyo wakati fulani katika maisha yako? Swali linalofuata: unamfahamu mtu aliye na moto kwa ajili ya Yesu maisha yake yote? Nimeona watu wengi ambao "wanatiwa moto" mwanzoni, lakini sikumbuki yeyote anayedumisha kiwango chao cha awali. Kwa nini hivyo? Je, hiyo ni sehemu ya kawaida ya utume wetu wa Kikristo? Je, hiyo ni sambamba na mapenzi ya Mungu? Tunapoitwa na Yesu katika utume, anatutarajia tufanye nini? Hebu tujivinjari tena kwenye Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza.

I. Washirika katika Utume

A. Soma Matendo 1:1-3. Yesu alifanya nini baada ya ufufuo wake? (Alikaa na wanafunzi wake kwa siku 40 akiwathibitishia kwamba kwa hakika alikuwa hai na kuwafundisha kuhusu Ufalme wa Mungu

B. Soma Matendo 1:4-6. Ni nani ambaye angefanya kazi na wanafunzi katika siku zijazo? (Roho Mtakatifu.)

1. Unafikiria nini kuhusu swali la wanafunzi katika Matendo 1:6?

a. Unafikiri liliulizwa lini? (Kumbuka ya kwamba hivi punde tu tumesoma katika Matendo 1:3 kwamba katika siku 40 Yesu aliongea nao kuhusu Ufalme wake. Natumaini hili swali lilikuwa mwanzoni mwa zile siku 40 na siyo mwishoni.)

C. Soma Matendo 1:7-8. Kwa kuzingatia msingi huu, wanafunzi watapaswa kushuhudia kitu gani? (Kwamba Yesu amefufuka na kwamba ana ufalme ujao.)

1. Je, huo ndio utume wetu leo? Maneno haya waliambiwa wanafunzi wakati huo, kama unadhani bado yanatumika, elezea kwa nini.

2. Je, walikuwa na uwezo wa kufanya kazi peke yao ? (Hapana. Walipewa maelekezo kamilifu kusubiri hadi pale watakapobatizwa kwa Roho Mtakatifu.)

a. Je, hilo pia ni hitaji leo? Je, lazima tusubiri hadi Roho Mtakatifu aje kufanya kazi pamoja nasi katika utume wetu?

(1) Je, ni nini kuhusu watu wanaosema kuwa wakati wa Roho Mtakatifu ukingali sasa katika nguvu umepita? Wana aina gani ya utume?

D. Soma Matendo 1:12-14. Walifanya nini kujiandaa na utume wao? (Walisali pamoja. Nadhani jukumu linabakia kuwa hilo hilo . Nadhani njia ya kutekeleza jukumu inabakia kuwa ile ile. Hatuwezi kujihusisha kikamilifu katika utume bila ya Roho Mtakatifu. Kama hatuna uhakika kuwa Roho Mtakatifu ni sehemu ya utume wetu, tunahitaji kusali kwa ari na hamasa ili tuweze kuzatitiwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya utume.)

II. Utume na utafutaji kipato

A. Je, "moto" unapoa pale tunapobaini kuwa tunatakiwa kutoka na kuweza kustahimili maisha

1. Au, kustahimili maisha ni sehemu ya njia ambayo kwayo tunafanya utume wetu

B. Soma Matendo 18:1-4. Je, Paulo alijihusisha na kuhubiri wakati wote? (Siyo katika mafungu haya. Yanatupatia picha kuwa walikuwa wakishona hema katika siku za wiki na kuhubiri siku ya Sabato.)

C. Soma Matendo 18:5. Je, sasa Paulo ametingwa/amesongwa kwa namna gani? Sasa amejihusisha na kuhubiri wakati wote.

D. Je, Paulo alikuwa na moto mdogo alipokuwa akihubiri wakati wa wikendi kuliko pale alipokuwa akihubiri wakati wote? (Natia shaka. Kufikia lengo la mahitaji yake ya kila siku ilikuwa ni sehemu ya kazi zake za jumla.)

E. Soma 2 Wathesalonike 3:6-10. Je, kazi isiyohusiana na masuala ya dini ni jukumu la kidini? (Paulo anasema kwamba kwa kuwa alijishughulisha/alijihusisha na utume alikuwa na haki ya "msaada" kutoka kwa Wakristo wenzake. Wakati huo huo anasema kuwa jumuiya ya Kikristo ina jukumu la kidini la kufanya. Kwa hiyo, wasingeweza wote kujihusisha katika utume.)

1. Hebu tuangalie kivitendo kuhusu suala hili. Unawafahamu watu katika kazi ambao kamwe hawawezi kwenda katika kanisa lolote

2. Je, una majirani wowote au mtu yeyote unayemfahamu lakini asiye rafiki wako wa karibu ambao kamwe hawawezi kwenda kanisani? ( Kama jibu ni "ndiyo," basi utume wako ni kuwafikia watu hawa kwa maisha ya mfano na yenye kuongozwa na Roho. Angalia Yohana 14:26)

F. Soma Tito 2:7-8. Ni kipengele gani katika maisha yako ambacho ni utume? (Kila tukifanyacho kinatoa ushawishi/athari kwa wema au kwa uovu. Utume wetu ni kuangalia asili ya ushawishi wetu, na kupitia uwezo/nguvu ya Roho Mtakatifu kutafuta kuufanya ushawishi wetu kuwa chanya katika kila Nyanja.)


 

III. Ujumbe Katika Utume

A. Soma 1 Wakorintho 1:18. Biblia inasema kuwa ujumbe wetu ni upi? (Msalaba.)

1. Tatizo la ujumbe wetu ni nini? (Neno linalichukulia kuwa ni upuuuzi.)

2. Tuliamua awali kuwa wanafunzi (na sisi pia) walipaswa kushuhudia ufufuo wa Yesu na ufalme wake ujao. Je, hilo ni sawia na ujumbe wetu kuwa msalaba? (Ndiyo. Msalaba na ufufuo wa Yesu unaonyesha fursa yetu kwa ajili ya msamaha wa dhambi na uzima wa milele.)

B. Soma 1 Wakorontho 1:19-21. Je, kuna habari njema katika kuhubiri "upuuzi"? (Huhitaji kuwa mwenye kipaji kushirikiana na wengine habari hii.)

C. Soma 1 Wakorintho 1:22-25. Je, tunahitaji miujiza au mantiki ili kusaidia kupeleka ujumbe? ( Kama unavyofahamu, napenda kutumia mantiki-kwa sababu nafikiri inasaidia kuendeleza injili. Lakini si mantiki wala miujiza iliyo muhimu katika ujumbe wetu: Yesu alisulubiwa.)

1. Kwa nini ujumbe wetu ni kwamba Yesu alisulubiwa? Kwa nini siyo matendo mazuri? Kwa nini siyo Sabato? Kwa nini siyo tabia nzuri za kula chakula? Kwa nini siyo mazoezi, siyo uvutaji sigara, au ufungaji wa mkanda wa usalama kwenye chombo cha usafiri? (Yesu kusulubiwa ni utimilivu wa huduma za patakatifu. Yeye ni Mwana-kondoo wa Mungu azichuaye dhambi zetu. Yohana 1:29. Hakuna kitu kingine chochote kituondoleacho dhambi zetu. Kafara ya Yesu ndiyo msingi wa ujumbe wetu. Kuna mawazo mengine mazuri, yenye kuleta mantiki na ya muhimu, lakini kiini cha ujumbe wetu ni msalaba.)

D. Soma 1 Wakorintho 1:26-27. Kwa nini Mungu anachagua wachezaji "dhaifu"? Anataka dunia ionekane mbaya? Kwa nini hilo ndilo lengo? (Ujumbe wetu ni Kristo, siyo sisi. Unaweza kuona wazo? Msalaba, siyo matendo yetu, ndio kitovu/kiini chetu. Kwa nini? Kwa sababu msalaba unaelekeza kile Mungu alichofanya, siyo kile tulichofanya. Wale walio na uwezo/nguvu, akili, msukumo/ushawishi, mwonekano mzuri hawana faida katika utume. Kwa hakika, wanaweza kuwa na hasara kwa sababu lengo linatakiwa liwe juu ya Mungu, siyo kwetu sisi wenyewe.)

1. Soma 1 Wakorintho 1:28-31. Je, hiyo inamaanisha kuwa watu werevu na wenye ushawishi hawastahili kufanya utume? (Angalia aliyeandika maneno haya-Paulo, mtu aliyefundishwa kwa hali ya juu, mtu mwerevu sana . Nadhani dhana ya Paulo ni kwamba kila mmoja anastahili kufanya utume ili mradi tu wanampa Mungu utukufu na kumfanya kuwa kitovu cha utume. Mungu hahitaji utukufu wa mwanadamu ili kazi yake iweze kufanyika. Anahitaji tu washirika wenye kupenda, wale wanaotambua uwezo na utukufu kumwendea/kumrudia Mungu.)

E. Katika siku ambazo nilikuwa na ushawishi mkubwa juu ya aliyehubiri katika mimbari ya kanisa langu, ningesema kuwa huduma ya kuabudu "siyo saa ya wasiokuwa na ujuzi," ikimaanisha kwamba watu ambao hawajajiandaa, wenye ukosefui wa mahitaji wa vitu vya kuhubiria na kwa hakika watu ambao hawana uzoefu wasiruhusiwe kuhubiri. Muda wa washiriki kanisani siku ya Sabato ulikuwa mdogo na wa thamani na sikutaka upotezwe na mahubiri ya ajabu ajabu. Soma 1 Wakorintho 2:1-5. Je, sikuwa sahihi? (Sistahili kujibu, lakini angalia aina ya hubiri ambalo lingekuja kutoka kwenye "kielelezo cha uwezo wa Roho." Roho Mtakatifu si yule asiyekuwa na maarifa, na kama Roho yu ndani yako, basi hata wewe hutokuwa usiye na maarifa pia.)

F. Rafiki, je, utauchukulia utume: katika ushirika na Roho Mtakatifu utashirikiana habari njema kuhusu Mwana-kondoo wa Mungu na ufalme wake ujao?


 

IV. Wiki ijayo: Tunaanza mfululizo mpya kuhusu waraka wa Yohana. Nausibiria kwa hamu!

No comments:

Post a Comment