Friday, June 12, 2009

JUMUIYA


(1 Petro 2, 1 Timotheo 5)

Maisha ya Mkristo: Somo la 12

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk

Utangulizi: Mjomba wangu alikuwa mtu wa kimungu. Akiwa amezaliwa muda mfupi tu baada ya kuanza kwa karne, alitumia muda wa maisha yake yote kama mchungaji na mtawala katika Kanisa la Jeshi la Wokovu. Siku moja nilimuuliza kuwa ni mabadiliko gani aliyoyaona katika jumuiya ya Kikristo katika miaka kadhaa iliyopita. Aliniambia kwamba televisheni ilichukua nafasi ya kanisa kama kituo cha Jumuiya. Kabla ya kuingia kwa televisheni, makanisa (na ninadhani sehemu za kuuzia vinywaji na vileo) yalikuwa ndio mtazamo wa mjamiiko (mwingiliano) wa kijamii. Sasa, alisema, watu wanakaa nyumbani na kufurahia jumuiya kupitia kwenye televisheni. Kama angekuwa bado yu hai leo, nadhani angeita mtandao (intaneti) na simu za mikononi kuwa jumuiya ya kizazi kijacho. Je, Mungu ana mpango gani kwa ajili ya jumuiya? Ni nini lililo lengo lake kwa wale wamfuatao? Je, teknolojia ni msaada au ni kikwazo? Je, kanisa litajirejea upya? Hebu tuingie katika somo letu na kubaini kile ambacho Biblia inasema kuhusu Jumuiya!

I. Taifa Takatifu.

A. Soma 1 Petro 2:4-5. "Jiwe Lililo Hai" ni nani? (Petro anamwongelea Yesu.)

1. Je, Petro anaongelea Jumuiya ya namna fulani? (Ndiyo.)

a. Matofali ya ujenzi wa jumuiya ni yapi? (Sisi ndiyo hayo matofali! Sisi ni "mawe yanayoishi.")

b. Lengo la Jumuiya yetu ni nini? (Sisi tu makuhani. Makuhani walimwakilisha Mungu kwa watu.)

(1) Fungu linasema kuwa tunatoa "dhabihu za roho." Inamaanisha nini kuwa tu aina fulani ya kuhani tukitoa aina fulani ya dhabihu? (Nafikiri inamaanisha kuwa tunakubali dhabihu ya Yesu kwa niaba yetu kwa ajili ya dhambi zetu, na tunawaambia wengine kuhusu hilo.)

B. Soma 1 Petro 2:6. Ni uhusiano upi uliopo kati ya Jiwe Lililo Hai na "mawe yaliyo hai?" (Yesu, Jiwe Lililo Hai, ni jiwe la pembeni la jengo linalofanywa na sisi mawe yaliyo hai. Yesu ndiye anayetupanga. Anayaongoza maisha yetu. Kama tunaamini njia yake, kamwe hatutaaibishwa).

1. Soma Yohana 14:6. Ni wajibu gani mwingine alionao Yesu katika Jumuiya? (Yesu siyo tu "Jiwe la Pembeni" la jumuiya yetu, yeye pia ni "Mlango" wa kuelekea kwenye jumuiya. Jumuiya yetu imejengwa katika Yesu.)

C. Je, teknolojia inasababisha matatizo mengine ya dhahiri katika jumuiya hii? (Haipaswi kufanya hivyo. Teknolojia husaidia mawasiliano. Kwa hiyo, kama sisi "mawe yaliyo hai" tunajengwa pamoja kumtegemea Yesu, mawasiliano bora yanapaswa kusaidia kuwa na mjengo bora.)

1. Je, Teknolojia yaweza kuwa tatizo? (Ndiyo. Kama ilitusababisha kujenga kwenye kitu kingine tofauti na Jiwe Lililo Hai. Inatupatia kiwango cha usiri ndani ya jumuiya ambayo inatupatia ukomo wa uwajibikaji.)

2. Watu wengi wanaopitiapitia mtandao (intaneti) wana sehemu ya "historia". Jiulize kama ungependa jamii yako ipelekewe mabadiliko ya papo kwa papo yatokanayo na historia ya upitiajipitiaji wako wa intaneti?

D. Soma 1 Petro 2:7-8. Je, Jiwe Linaloishi laweza kuwa tatizo? (Siyo ya msaada kwa wale wanaotaka kutomtii Yesu. Inasababisha kwa wao kujikwaa na kuanguka.)

1. Kwa nini? Warumi 9:33 inajaili kuhusu suala hili. Wale ambao wanashikilia haki kupitia matendo hawawezi kukubali kwa imani kunakotolewa na Yesu. Sisi ni jumuiya iliyojengwa juu ya imani.)

E. Soma 1 Petro 2:9. Ni nini azma ya jumuiya yetu iliyojengwa juu ya Yesu?

1. Kwa nini tunaitwa kuwa "wazao wateule"? Je, haya siyo maelezo juu ya watu wa Uyahudi? (Ilikuwa wamwakilishe Mungu duniani. Lakini, walishindwa kufikia lengo la Mungu kwao. Leo,kanisa humwakilisha Mungu kwa dunia.)

2. Tunamsifu nani? (Yesu-ambaye alituita kutoka gizani kwenda mwangani. Azma ya jumuiya yetu kueneza mwanga juu ya zawadi ya Mungu ya rehema duniani.)

F. Soma 1 Petro 2:11. Ni mtazamo wa aina gani unaopaswa kuwepo katika wanajumuiya wa Yesu? (Tunapaswa kujizuia na tamaa za dhambi. Tunapaswa kujichukulia kama "wapitaji na wageni katika dunia hii.")

1. Kwa nini? (Matamanio ya dhambi huleta vita dhidi ya roho zetu.)

2. Tafakari kuhusu historia ya upitiajipitiaji wako wa intaneti. Fikiria kuhusu usengenyaji wako uliopita. Wawezaje kudhibiti matamanio yako?

G. Ni kipengele muhimu kiasi gani kwa jumuiya kuwa na maisha sahihi? Sote tunafahamu juu ya wakristo ambao "walianguka kutoka kwenye mkokoteni" pale inapokuja kwenye kuishi maisha yaliyo sahihi/makamilifu. Halikuwakinga. (Jumuiya ya Kikristo kwa hakika siyo dhamana, bali inasaidia kuishi maisha makamilifu/yaliyo sahihi.)

1. Ninafikiria kuhusu ushawishi wa jumuiya pale nilipokuwa mtoto. Sehemu ya kuuzia magazeti ya Johnson ndipo baba yangu, mtu mashuhuri katika jumuiya, alipokuwa akisimama na kununua gazeti kila siku usiku. Palikuwa pia ni mahala pekee katika jumuiya ile nilipopafahamu ambapo palikuwa panauza picha za wanawake waliokuwa uchi. Uwezekano wa baba yangu kununua mojawapo wa magazeti yale mbele ya "jumuiya" yake ilikuwa ni sawa na baba yangu kuvua nguo zake katika duka/kituo kile!

H. Soma Petro 2:12. Jumuiya inapaswa siyo tu kuwasaidia wanajumuiya, bali pia kuwa shahidi kwa wapagani. Je, wapagani watakubaliana kuwa na muktadha wa kuvutia wa jumuiya ya Kikristo? (Hapana. Wanatutuhumu kwa kutenda mabaya.)

II. Kuitegemeza Jumuiya

A. Soma Yakobo 1:27. Yakobo ni mwandishi anayesisitiza kazi za Mkristo. (Mara nyingine huwa ninafikiri kuwa Yakobo na Paulo wangepaswa kushirikiana kwenye kitabu cha Biblia.)

B. Soma 1 Timotheo 5:3-4. Ni Jumuiya ya aina gani tuliyonayo ndani ya jumuiya kubwa ya Kikristo? (Jamaa [familia]-hata familia kubwa inayohusisha wanandugu.)

1. Soma 1 Timotheo 5:7-8. Kwa nini mtu awe mbaya zaidi ya yule asiyeamini kama hakuisaidia familia yake? ( Kama huwapendi na kuwasaidia wale ambao wana hitaji kubwa la mguso wako, wawezaje kuwapenda na kuwasaidia wale usiowafahamu? Zingatia 1 Yohana 4:20-2.)

C. Soma 1 Timotheo 5:9-10. Wasomi wanatofautiana kwa kile inachomaanishwa kwa "orodha ya wajane." Wengine wanadhani kuwa hawa ni waajiriwa wa kanisa. Katika kukusaidia kuamua, soma Matendo ya Mitume 6:1 na 1 Timotheo 5:16. Unafikiria nini?

1. Baada ya waaminio walioelezewa katika Matendo ya Mitume 6 kuwa wamejipanga sawa sawa, unafikiri kuwa walijuaje wapi pa kugawa chakula? (Walikuwa na orodha! Nadhani "orodha ya wajane" katika 1 Timotheo 5:9 ni wale wajane wanaosaidiwa na kanisa. Mashaka yoyote katika mawazo yangu yanafutwa pale ninaposoma 1 Timotheo 5:16.)

D. Angalia tena 1 Timotheo 5:9-10. Hili linatufundisha nini kuhusu umuhimu wa jumuiya katika kuamua nani wa kumsaidia?

1. Kazi ya mjane "anayestahili" inatufundisha nini kuhusu jumuiya? (Ni msaada kutoka pande zote mbili katika kundi kwa kiasi fulani.)

a. Je, hii ni kazi tu ya mjane? (Hii ni kazi yetu sote. Hii ni sehemu ya kuwa jumuiya.)

E. Soma 1 Timotheo 5:11-14. Je, twapaswa kumsaidia kila mtu anayeomba msaada-kila mtu anayetaka kuorodheshwa kwenye orodha ya wanaohitaji msaada? (Paulo anatufundisha kwamba tusiwatie watu moyo kutokuwa na chochote cha kufanya na hivyo kujiingiza kwenye matatizo.)

1. Je, hii ni sheria ambayo tunapaswa kuitumia kwa wale wote wanaoomba msaada wetu?

a. Soma Luka 6:30-31. Unayaelewaje mafungu haya?

2. Je, tuamueje kuhusu ni nani wa kumsaidia?

F. Mara mbili sasa, katika wiki tatu zilizopita, nilikuwa katika duka moja katika sehemu fulani maarufu nje ya mji na nilikutana na watu wazima (wasiokuwa walemavu) wakaniomba kuwa niwapatie fedha. Ningeweza kuwapatia fedha pasipo kuathiri bajeti yangu. Unafikiri kuwa ningefanya nini? (Rejea wiki iliyopita tulisoma (Mathayo 25:34-36) kwamba wenye haki waliwapatia msaada/mahitaji ya kimwili (nguo, chakula) na si fedha kwa walio wahitaji? Wiki hii tunaona Paulo anasema kuwasaidia wale wanaostahili na usitie moyo wasio na kazi/walegevu. Suala la kawaida linaonekana kutuhitaji sisi kuwa na ujuzi kuhusu mahitaji ya mtu kuomba/kuwa na uhitaji wa msaada. Ni rahisi tu kutoa fedha, lakini suluhisho lililo bora/kamilifu ni kuwa na taarifa sahihi kumhusu mtu husika.)

1. Baada ya kufikia hili suluhisho lenye kuleta mantiki, soma maneno ya Yesu katika Luka 6:35-36. Yesu anasema kuwa wema kwa wengine-hata wasioshukuru na waovu! Je, hii inamaanisha kuwa tunapaswa kuwasaidia ombaomba wavivu? (Inavyoonekana, ni kwa kiwango fulani.)

G. Kama ufumbuzi wa kiambato kwa jumuiya ni kuwasaidia wale walio wahitaji, na kujua wale wanaopaswa kusaidiwa, je, televisheni na teknolojia nyingine zina athari gani katika kazi hii? (Bila kukutana na washiriki wengine katika jumuiya ya makanisa yetu nje ya ibada rasmi, hatutakuwa na wazo kuhusu mahitaji yao au namba gani bora ya kusaidia. Inaonekana kuwa teknolojia ni kikwazo katika hilo .)

1. Ungependekeza kuwa ni namna gani ya "kutatua" hili? (Suluhisho bora ni kuwa na jumuiya ya kanisa kukutana pamoja katika vikundi vidogo vodogo kwa ajili ya kujifunza Biblia pamoja na masuala mengine. Hilo linatusaidia kufahamiana.)

a. Je, kuna tafsiri nyingine ya kiteknolojia ya hili? (Facebook? Je, ni nini kuhusu usomaji wa Biblia kwa kutumia Skype?)

H. Rafiki, je, upo katika "jumuiya" na Wakristo wengine? Kama sivyo, kwa nini usiungane na kundi la waaminio leo? Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yako.

III. Wiki ijayo: Mission.

Somo limrletwa kwetu na masatu Mgune






No comments:

Post a Comment