Friday, July 24, 2009

Somo la 5:Kutembea Nuruni: Kuyakana Mambo ya Ulimwengu


(1 Yohana 2)

1, 2 & 3 Yohana: Somo la 5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.

Utangulizi: Kuishi pembezoni mwa bahari inamaanisha kuwa natumia muda mwingi ufukweni kuliko nilivyokuwa nafanya huko nyuma. Mara kwa mara nawaona wanawake wa kiislam wakiwa ufukweni. Tofauti kati yao na watu wengine wa kawaida wanaotembelea ufukweni ni dhahiri. Inanikumbusha nilipokuwa kijana na washiriki wa kanisani kwangu walikuja siku ya Sabato karibu na fukwe za karibu za Ziwa Michigan. Mara kwa mara washiriki wa kanisa bado walikuwa wakivaa suti na mavazi ya kikanisa, wakati ambapo watu waliokuwa wakiota jua walikuwa vakivaa vitu tofauti kabisa. Somo letu la juma hili ni kuhusu "mambo ya ulimwengu." Je, mifano hii miwili ni ya kuyakana "mambo ya ulimwengu"? Is sticking out like a sore thumb God's goal for us? Au, hiyo ni kuifanya kauli ya wazi kwa ulimwengu? Hebu tujivinjari kwenye somo letu la Biblia na kuona kile ambacho Yohana anatufundisha kuhusu mambo ya ulimwengu!

  1. Watoto, Wanaume na Akina Baba
    1. Soma 1 Yohana 2:12-13. Yohana anasema anawaandikia watoto, akina baba na vijana. Je, hiyo ndiyo sababu tuna nyaraka tatu: Yohana wa kwanza, pili na tatu?
      1. Kama ndio hivyo, kwa nini Yohana anaonyesha makundi mengine mawili katika Yohana wa Kwanza? (Yohana hana waraka mwingine kwa kila kundi.)
      2. Je, Yohana ana ujumbe wa aina tatu tofauti kutegemeana na kundi linaloelezewa?
      3. Kwa nini wanawake wameachwa, yaani, hawakutajwa kwenye ujumbe? Je, wao tayari ni wenye haki?
    2. Hebu kwanza tuwaangalie watoto. Fungu linasema kwamba wamesamehewa dhambi zao na kwamba wamemjua baba. Je, hilo siyo kweli pia kwa makundi yote matatu? (Nafikiri Yohana anazungumzia waumini wapya, siyo watoto kikwelikweli. Muumini mpya anaweza asiwe na uelewa mpana wa injili. Hata hivyo muumini mpya ambaye alikuwa Myahudi aliyebadili dini ange "mjua Baba," ikimaanisha Mungu wa Agano la Kale. Muumini mpya angekuwa katika jukwaa la uelewa kwamba Yesu alikuwa kafara "mpya" ya dhambi. Sababu ambayo Yohana hawataji wanawake ni kwamba anaandika kuhusu kukomaa kiroho, siyo jinsia.)
    3. Tuna ujumbe gani kwa akina baba-Wakristo waliokomaa? ("Umemjua Yeye ambaye yupo tangu mwanzo.")
      1. Unadhani hili linamaanisha nini? (Kama tulivyoona hapo awali, hili linamrejea Yesu (Yohana 1 na 1 Yohana 1). Hawa ni Wakristo walio na uelewa wa Yesu.)
    4. Tuna ujumbe gani kwa "vijana?" (Wamemshinda mwovu.)
      1. Tunawezaje kusema kwamba mwanadamu yeyote "anamshinda mwovu?" (Hawa ni Wakristo wanaokua. Wanatambua kwamba Yesu amewasamehe dhambi, lakini wana mwendo wa kiroho kuelekea kwenye haki. Wanaweka lengo la kila siku la utii.)
    5. Soma 1 Yohana 2:14. Ni kitu gani kingine tunachojifunza kuhusu "vijana?" (Neno la Mungu hukaa ndani yao. Wanasoma neno la Mungu. Wanamtegemea Roho Mtakatifu.)
    6. Hebu tufanye tathmini: Yohana anawaandikia waumini wa madaraja yote ya ukomavu wa Kikristo. Anasifia  kila kundi katika maendeleo waliyoyafikia hadi sasa. Kinachofuata, tunageukia ujumbe wake kwa makundi yote.
  2. Kuipenda Dunia
    1. Soma 1 Yohana 2:15. Kila kitu ninachokijua na kukigusa na nilichokizoea kipo "duniani". Nawezaje nisikipende?
      1. Kwa kuwa tumeambiwa kuwa kuipenda dunia ni kinyume na kumpenda Mungu, unadhani inamaanisha nini kusema kuwa "dunia" na "chochote kilichomo duniani?"
    2. Soma 1 Yohana 2:16. Tunaona nini "duniani?" (uchu, tamaa ya mwili na kujisifu/kujigamba.)
      1. Je, "mambo" haya yamo "duniani?" (Hapana. Hii ni mitazamo kuhusu vitu fulani.)
      2. Hebu tuangalie hili kidogo. Kama Yohana anaongelea kuhusu mambo ya ulimwengu, je, anatufundisha kwamba mambo ya ulimwengu ni mtazamo au matarajio?
        1. Kama habari ndiyo hiyo, kuna uhusiano gani kati ya jinsi Mkristo anavyovyaa na mtizamo wa Mkristo?
          1. Hili linasema nini kuhusu "vazi la ufukweni" nililolielezea kwenye utangulizi? Je, kujivika, au kuvaa mavazi tofauti, ni kukataa/kukana mambo ya ulimwengu?
      3. Kama uchu, tamaa ya mwili na kujisifu/kujigamba ni mitizamo kuhusu vitu fulani, je, hiyo inamaanisha kuwa watu wasio na vitu (masikini) wanaweza kuwa wa dunia? (Kinyume chake ni kwamba wale wasio na vitu wanaweza kuwa na matatizo mengi kuhusiana na hili kuliko wale walio na vitu na kuamua kuwa "vitu" siyo vya msingi kihivyo.)
    3. Soma tena 1 Yohana 2:16. Kauli "cravings of sinful man," inatafsiriwa kuwa "tamaa ya mwili."  Hii inatusaidiaje kujua kile inachomaanisha? (Mtu aliye na tamaa hizi (hii "tamaa") ana mtazamo juu ya mambo ya kidunia.)
      1. Vipi kuhusu wewe? Una mtazamo wa kidunia? Unatamani vitu fulani? Unatamani ungekuwa na vitu fulani?
    4. Tulipokuwa tukielekea kanisani wiki iliyopita, mimi na mke wangu tulikuwa tukiongelea mambo ya mbeleni. Tunapanga kuuza nyumba yetu ya sasa na tulikuwa tunajadili kuhusu mahala pengine pazuri/bora pa kuishi. Mahala pazuri kwangu ni nyumba hii (hapa tunapotaka kupauza) karibu kabisa na ufukwe ambapo unaangalia ghuba ya Chesapeake na bahari ya Atlantiki. Gharama? Dola milioni 1.3. mke wangu angependa kuishi katika milima ya  Blue Ridge-takriban saa 3 kutoka ufukweni. Nikasema, "Kama tungekuwa na pesa za ziada kidogo tungejipanga"-ikimaanisha kwamba tungeweza kununua nyumba ya ufukweni na nyumba iliyopo katika milima ya Blue Ridge . Je, hizo ni "tamaa za mdhambi" na "tamaa za macho yake?" (Ndiyo! Angalao kama inaelekea kwenye hatua ya uchu na kutamani tofauti na kuchukulia kwamba mambo haya hayawezekani.)
    5. 1 Yohana 2:16 inamaanisha nini inaporejea "tamaa ya macho yake?" (Unataka kile unachokiona.)
      1. Kwa nini hili ni makosa? (Vitu vya kiroho kwa ujumla huwa havionekani. Vitu vya kiroho mara kwa mara huwa ni mahusiano. Kwa hiyo, unatamani juu ya mambo mabaya/yasiyostahili katika maisha.)
    6. 1 John 2:16 inarejea kitu gani inapoongelea "kusaidia kile alichonacho na akifanyacho?" (Huu ni mshale moyoni mwangu. Mara zote nimekuwa nikifurahia kuwa mwanasheria. Napenda kusema kuwa mimi ni mwalimu wa shule ya sheria kwa sababu inapendekeza kuwa mimi siyo mwanasheria tu, bali mwanasheria mwerevu. Hili ndilo linaonekana kwa hakika Yohana analishutumu kuwa la kidunia. Kama mtu yeyote anataka kuniokoa kwa kupendekeza tafsiri nyingine, nipo wazi kulisikiloiza! Kwa sasa ninatubu.)
  3. Mtazamo wa mbali
    1. Soma 1 Yohana 2:17. Kuna shida gani na aina hizo za matamanio? Haya mambo ya ulimwengu?
      1. Je, Yohana anasema kwamba mtazamo wa kidunia, kuwa na hisia kuhusu kuwa na "vitu" ni dhambi? Au tu ni kujishughulisha/kujifikirisha kipumbavu?
      2. Kama mtu hampendi Mungu, je, hiyo siyo ishara ya "dhambi?" (Yote haya yana mantiki kwangu. Kama tunajishughulisha na kupata vitu, basi hatujishughulishi na kumjua Mungu. Mathayo 6:24 inasema kwamba fedha ni bwana. Hatuwezi panda na kumtumikia Mungu na pesa. We cannot love and serve both God and money.)
      3. Umewahi kusikia msemo "ilikuwa nzuri wakati ambapo ilikaa kwa muda mrefu?" Je, linahusika hapa-kwenye kauli ya 1 Yohana 2:17? 
      4. Mungu anatupatia kitu gani kilicho bora sana? (Uzima wa milele! Vitu vya milele. Nadhani Yohana anajenga hoja kivitendo. Kile ulicho nacho na vile jinsi ulivyo sasa ni vya muda tu. Pale unapokufa, nani anakumbuka au anajali? Pesa yako inakwenda kwa mtu mwingine. Inaleta mantiki gani kujishughulisha na kitu ambacho kwa hakika utakipoteza? Kwa upande mwingine, Mungu anatupatia vitu vya milele na sifa njema.)
    2. Una ufahamu wa kiasi gani kuhusu babu zako wa mbali sana (mababu wa babu zako)? (Nilipokuwa ninaandika somo hili, mke wangu alipata na kunitumia kipande cha picha ya video kuhusu kujiuzulu kwa baba yangu katika wadhifa wake wa mwisho. Kitini hicho kilikuwa na kichwa cha habari kikubwa na picha ikionyesha kwamba baba yangu alikuwa mtu mzuri sana wa sura. Lakini kitini hicho ni kama vile hakikuelezea chochote kuhusu kazi yake au mafanikio yake. Badala yake, kilitaarifu kuwa alikuwa na ugonjwa wa moyo, kikaonyesha kiasi alichopata (pesa) na kwamba walikuwa watafuta mtu mbadala. Kile tulichonacho na kile tunachokifanya, yote ni ya muda tu!)
    3. Rafiki, vipi kukuhusu wewe? Unatizamia umilele au mambo ya dunia hii? Kwa nini usiamue leo kutizamia kwenye mambo ambayo hayataisha kamwe! Habari gani kuhusu kuwa wa "kimbingu" badala yaw a "kidunia?"
  4. Wiki Ijayo: Kutembea Nuruni: Kuwakataa Wapinga Kristo.


 

Kama ilivyofasiriwa na Mgune Masatu.

Friday, July 17, 2009

Somo la 4: Kutembea Nuruni: Kutunza Amri Zake

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk. Muombe Roho Mtakatifu akuongoze ujifunzapo somo hili.

 
 

Utangulizi: Mojawapo ya majukumu yangu kama mwanasheria ni kuthibitisha mada za kesi za wateja wangu. Ninapokuwa nikitetea kesi za kidini, kitu cha kwanza ni kuthibitisha kwamba mteja wangu ana "imani ya kidini ya dhati." Wewe ungefanyaje kuhusiana na hilo ? Utathibitishaje kwa hakimu, asiyemfahamu mteja wako, kile kilichomo moyoni mwa mteja wako? Ninatumia matendo ya mteja wangu kuthibitisha kile kilichomo moyoni mwake. Je, njia yangu ni njia ya Mungu? Matendo yetu yana uhusiano gani na kile kilichomo mioyoni mwetu? Hebu tujivinjari kwenye somo letu na kubaini kile ambacho Mungu anakisema kuhusu hili!


 

  1. Lengo
    1. Soma 1 Yohana 2:1. Wiki iliyopita tulijifunza kwamba wale "wanaotembea katika nuru" wana dhambi maishani mwao. (1 John 1:7-8) Je, hilo linakanusha matendo yangu = nadaharia ya moyo (heart theory)?
      1. Je, dhambi hiyo ni sawa tu kwa Yohana? Ni vipi kuhusiana na hilo kwa Mungu? Je, ni sahihi kutembea katika njia ya nuru ukiambatana na mzigo huu wa dhambi?
      2. Yohana anasema kuwa lengo ni nini? (1 Yohana 2:1: "Nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi." Lengo ni kuachana na dhambi.)
      3. Je, hili ni lengo halisi? Nini kinatokea endapo tutakosea? (Yohana anasema kuwa tunaye Yesu mtetezi wetu. Inafanana kabisa/Yesu anaonekana kama mwanasheria!)
    2. Angalia tena 1 Yohana 2:1. Yesu "anatuteteaje" mbele za Baba? Kwa kujenga hoja kwamba kila mtu anatenda dhambi, na kwamba Mungu asiangalie dhambi mojamoja?
      1. Je, Yesu anajenga hoja kwamba kile tulichokifanya hakikuwa dhambi haswa?
    3. Soma 1 Yohana 1:10. Ni watu wa aina gani tulioamua wiki iliyopita kuwa ndio walioelezewa hapa? (Haya ni makundi mawili: Kwanza, wale wanaodai kuwa wamefikia kiwango cha ukamilifu na kwamba hawana dhambi. Pili, wale wanaosema kuwa hawatendi dhambi sasa na kamwe hawajawahi kutenda dhambi kwa sababu dhambi kwa hakika haipo kwa ajili ya Wakristo. Inaleta mantiki kwamba Yesu asingekuwa anarudia kubadilika kwa hizi hoja mbili potofu.)
    4. Unafikiri watu walioelezewa katika 1 Yohana 1:10 ndio wale wale ambao Yohana anazungumza nao katika 1 Yohana 2:1? (Hapana. Yohana anaanza kwa kusema "watoto wangu wadogo." Haendelei kuzungumza na kundi la watu wale wale aliokuwa akiwaongelea katika fungu la 10. Alisema kuwa watu walioelezewa kwenye fungu la 10 walikuwa wanamfanya Mungu kuwa mwongo na neno la Mungu halina nafasi maishani mwao. Yohana amegeukia kundi lingine la watu wanaoutafuta ukweli. Hawa ni watu wanaotembea kwenye njia
      ya nuru. Hawa ni watu wanaotaka mioyo yao na matendo yao kushabihiana/kuendana.)

    5. Sasa kwamba tumeshajadili kile tunachofikiri Yesu anaweza kukijengea hoja, hebu tusome 1 Yohana 2:2 na kujaribu kuona kama tunaweza kubaini kile ambacho kwa hakika anakijengea hoja. Ni hoja ya aina gani inapendekezwa ambayo Yesu anaifanya badala yetu?
      1. Fikiria kwamba umeburuzwa mbele ya hakimu na unashitakiwa kwa kufanya kosa la jinai. Na pindi usimamapo na kujaribu kujiweka vizuri (na kutokuwa kwako na hatia) mara unamsikia wakili wako akianza kujenga hoja zake: "Mheshimiwa, mteja wangu ana hatia, tena ana hatia sana….." Ungesema nini?
        1. Je, huo ndio utetezi wa Yesu kwa ajili yetu? (Ndiyo! Utetezi wake ni kwamba tuna hatia sana , lakini tayari amekwishalipa adhabu. Habishani dhidi ya hatia yetu. Anabisha dhidi ya adhabu nayowekwa juu yetu.)
      2. Katika muktadha wa hoja ya Yesu (wakili wako), ni vipi juhudi zetu za kuficha na kukataa dhambi zetu zinaonekana? Fikiria hatua ya hakimu kama ungeanza kupingana na wakili wako na kauli ya kuudhi, "Sina hatia! Naishi maisha makamilifu! Matatizo yoyote ninayoweza kuwa nayo siwajibiki nayo. Ni makosa ya kurithi niliyoyapata kutoka kwa baba yangu na mama yangu!"
    6. Tumeamua dakika chache zilizopita kuwa 1 Yohana 2:1 imeelekezwa kwa "wale walio katika njia yenye nuru." Je,hili liko sawa na 1 Yohana 2:2? (Kafara ya Yesu ni "kwa ajili ya dhambi za dunia yote." Kafara yake inaweza isikubaliwe na wote, lakini aliyatoa maisha yake kwa kila mtu.)
    7. Fikiria hili: Kwa nini Yohana anamuwianisha Yesu kama anayetutetea au anayepigania nafsi yetu kwa Mungu? Je, Mungu Baba anahitaji kushawishiwa? Je, hii ni aina fulani ya mjadala ambayo tunatumai kuwa Yesu anashinda?
    8. Soma Yohana 16:26-27 ambapo Yesu anasema kuwa "wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda….." Hili linalinganaje na uhitaji wa wakili? (Utetezi wa Yesu ni kinyume na matakwa ya sheria, na siyo matakwa ya uhasama (kwetu, badala ya juu ya dhambi) ya Baba. Kile ambacho Yesu ametutendea ni zaidi ya maneno ya kuelezeka, na ukweli kwamba Yesu anajitokeza mbele kwa niaba yetu hufanya utetezi wetu kuwa dhahiri.
  2. Kumjua Mungu
    1. Soma 1 Yohana 2:3-4. Mara kwa mara mtu fulani huniuliza kama namfahamu mtu fulani muhimu. (Kwa kweli, kwa ujumla huwa ni kinyume,huwa nina shauku kuwaelezea wengine kama namfahamu mtu yeyote ambaye si wa muhimu. Ina maanisha nini "kumjua" mtu fulani? Yohana anamaanisha nini anapotuandikia sisi kuwa anamjua Yesu? (Kumjua mtu fulani inamaanisha kuwa unafahamu kitu fulani kumhusu.)
      1. Kama hili ni kweli, sasa kwa nini tena utii wa sheria ya Mungu ni "kipimo cha uhalisia" wa kumjua Mungu? (Kimantiki, lazima imaanishe kuwa kuna muunganiko thabiti kati ya kumjua Yesu na kujua amri zake.)
      2. Je, hili linathibitisha mtazamo wangu wa kimahakama: kwamba matendo ya mteja wangu yanaelekea kuonyesha endapo mteja "anamjua" Yesu? Ana moyo kwa ajili ya Yesu?
    2. Kwa nini Yohana anasema kuwa tumheshimu Yesu?  Motisha yetu ni nini? (Tunamjua.)
      1. Kwa nini Yohana hasemi tutii kwa sababu tunajua kanuni?
      2. Kwa Yohana hasemi  tutii kwa sababu tunamcha Mungu?
      3. Kwa nini Yohana hasemi  tutii kwa sababu tumepitia uzoefu wa changamoto ngumu kabisa ama uzoefu wa raha na hali njema
    3. Je, hii ni kanuni ya Ulimwengu? Ya kwamba tutii kile tunachokijua?
      1. Kama utasema, "ndiyo," jiulize kuwa ulitumia muda gani kumjua Mungu wiki iliyopita ukilinganisha na kulijua joka likiongea kupitia kwenye televisheni?  
    4. Kama utasema, "siyo kweli, Bruce, kwamba natii kila kitu ninachokijua," basi kwa nini kumjua Mungu inamaanisha kuwa tumtii? (Hii inasema chemsha bongo fulani kuhusu Mungu. Pendo lake na tabia yake ni kwamba kumjua hutufanya tutake kutii!)
    5. Marafiki zangu, hili ni jambo linaloua: hatuwezi kumtii Mungu isipokuwa kama tunamjua. Upande mwingine wa mlinganyo huu ni makini zaidi: hatumjui kama hatumtii.)
    6. Soma 1 Yohana 2:5. Unafikiri Yohana anamaanisha nini pale anaposema kuwa upendo wa Mungu umekamilika kwa yeyote yule anayetii? (Ukristo siyo wa kinadharia. Siyo uelewa wa kanuni  zinazodhanika ambazo hazileti utofauti wa kivitendo katika maisha yetu. Upendo wa Mungu unakamilika kwetu pale tunaporuhusu mapenzi yake yabadilishe matendo yetu.)
    7. Soma 1 Yohana 2:6. Inamaanisha nini "kutembea" kama Yesu alivyoenenda? Je, inamaanisha kuwa:
      1. Hatuna fedha?
      2. Hatuna mke/mume (mwenza)?
      3. Tunahubiri? (Yohana kwa hakika, kwa uwiano sahihi, anaelekeza dhana kuwa utii ni wa msingi sana . Haongelei kuhusu masuala fulani ya maisha ya Yesu, anaongelea kuhusu dhamira ya Yesu ya kumtii Baba yake na kuakisi mapenzi ya Baba yake. Mioyo yetu na matendo yetu ina uhusiano.)
  3. Matokeo ya Kumjua Mungu.
    1. Soma 1 Yohana 2:7-8. Je, Yohana anatukumbushia kuhusu amri ya zamani au anatuambia kuhusu amri mpya? Yohana anaanza kwa kile kinachoonekana kama vile ana kipingamizi: "siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani. Labda ni aina fulani ya amri mpya." Ni ipi hii? (Ni amri ya zamani ambayo haitambuliki kwa dhahiri hapo kabla kwa sababu mwanga mpya unaturuhusu kuiona.)
      1. Umewahi kupata kitu cha kale, ukakisafisha, na kudhani kuwa kimeonekana tofauti kabisa? Kipya kabisa?
    2. Soma 1 Yohana 2:9-11. Je, hii sheria ya kale iliyofanywa kuwa mpya ni ipi? (Kuwapenda Wakristo wenzetu).
      1. Imewezwaje kufanywa upya? Asili ya mwanga mpya ni ipi? (Hujui namna ya kupenda, Yohana anasema, hadi mmeona jinsi Yesu alivyopenda! Yesu "alisafisha" upendo wa kale na dhana/wazo la utii kutupatia mfano wa kile kilichodhamiriwa. Chukulia mifano miwili: 1) Mkono uliopooza uliponywa siku ya Sabato (Mathayo 12); na, 2) Mjadala wa Yesu kuhusu umuhimu wa kile kitokacho kinywani badala ya kile kiingiacho kinywani (Mathayo 15).)
    3. Rafiki, unapima vipi uhalisia wa 1 Yohana 2:9-11? Matendo yako yanasema nini kuhusu moyo wako? Je, unamchukia mtu yeyote? Una vinyongo na watu? Mtizamo wako ni upi kwa familia ya Mungu? Jibu la maswali haya linaonyesha kama upo kwenye njia yenye "nuru" au njia yenye " giza ".

 
 

  1. Wiki Ijayo: Kutembea Nuruni: Kuyakana Mambo ya Ulimwengu.


 

Friday, July 10, 2009

Lesoni ya 3: Kutembea Nuruni: Kugeuka na Kuacha Dhambi



(1 Yohana 1)


Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.

Utangulizi: "Ina tatizo gani?" Umeshawahi kujiuliza hilo swali pale ulipotaka kufanya jambo lenye mashaka (linaloweza kujadiliwa)? Je, watoto wako wamekuuliza hilo swali pale walipotaka kufanya jambo ulilowazuia? Biblia inafundisha kwamba kuna wigo mpana wa maamuzi ambao hauhusishi dhambi. Wakristo wanaweza kutokubaliana kwa kutumia akili (kwa kutafakari kwa makini) kama baadhi ya matendo ni dhambi, na kila upande unaweza kuwa sawa. (Angalia Warumi 14.) Wakati huo huo, Yohana anatufundisha kuhusu umuhimu wa maamuzi yetu yote. Analinganisha maisha na kufanya matembezi. Je, kila maamuzi maishani yanatupeleka karibu zaidi na haki au karibu zaidi na dhambi? Hebu tujivinjari katika somo letu na kubaini! Tunaweza kuamua kama "Ina tatizo gani?" ni swali sahihi au la.

  1. Nuru = Mungu
    1. Soma 1 Yohana 1:5. Wiki iliyopita tulijadili kwa nini Yesu anaelezewa kama "Neno la Uzima." Sasa katika 1 Yohana 1:5 tuna neno jipya kumhusu Yesu, "Nuru." Unafikiri kwa nini Mungu anaelezewa kama "Nuru?" Kwa nini neno hili lahusika au ni maelezo sahihi kumhusu Mungu?
      1. Nini kinakujia mawazoni pale unapofikiri kuhusu nuru? (Nguvu/uwezo. Uwezo wa kuona. Jukumu. Uwazi.)
      2. Yesu anasema "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe." Yohana 8:12. Hii inapendekeza nini kuhusu asili ya "nuru" ya Mungu? (Ya kwamba inatusaidia kuelewa ukweli kutokana na uongo [wema kutoka kwenye uovu]).
    2. Wiki iliyopita tulijadili kwamba sababu moja kwa nini "Neno" yalikuwa ndio maelezo sahihi kumhusu Yesu ni kwamba aliumba ulimwengu kwa kutamka tu, kwa "neno". Tukitafakari kwenye uumbaji tena, nini kiliumbwa kwanza? (Mungu alitamka "nuru" nayo ikawa. Mwanzo 1:3). 
      1. Unaona uhusiano kati ya tendo la kwanza la Yesu la uumbaji na kile anachoitwa? (Nuru humwelezea Mungu. Alituumba kwa mfano wake. Kwa hiyo ni kawaida kwamba pale alipoanza "kutamka" uumbaji alianza na nuru.)
    3. Angalia tena 1 Yohana 1:5. Yohana anasema kwamba hamna giza lolote ndani ya Mungu. Kwa nini hili ni muhimu? Kwa nini kipengele hiki kiongezwe? (Sababu tatu: Kwanza , miungu iliyokuwepo wakati huo ilikuwa na upande muovu pia. Ilikupasa kuwa makini jinsi ulivyohusiana nayo kwa sababu ungeweza kuamsha hisia za hasira tena isiyo ya haki. Pili, tunahitaji kujua asili ya ushirika wetu na Yesu. Sasa tunashirikiana na "mtu fulani" ambaye ni nuru kabisa – mwema kabisa. Tatu, uovu hautoki kwa Mungu.)
  2. Uchaguzi
    1. Soma 1 Yohana 1:6-7. Tafakari ya kwamba unatembea kwenye msitu mdogo (sehemu yenye miti mingi) na unafika njia panda. Unatakiwa kuchagua njia ya kufuata. Katika haya mafungu mawili Yohana anafafanua njia panda katika maisha. Kwa mujibu wa Yohana, ni chaguzi gani mbili zilizopo? (Tunaweza kuchagua nuru au tunaweza kuchagua giza .)
      1. Kwa namna nyingine, Yohana anaelezeaje chaguzi hizi? (Mwishoni mwa fungu la 6 linarejea jambo "ukweli." Kwa hiyo, tuna uchaguzi wa "kweli" ama "uongo.")
      2. Ni maneno gani mengine ungeweza kuyatumia kuelezea chaguzi hizi? (Vipi tukitumia "wema/uovu," njema/mbaya," "haki/isiyokuwa haki?")
    2. Angalia tena 1 Yohana 1:5. Kwa mujibu wa Yohana, ni nani ambaye ni muasisi wa hili wazo la kuwa na chaguzi mbili za maisha barabarani? (Yohana anaweka kijisehemu kidogo katika fungu la 5 kuhusu chanzo cha ujumbe wake. Anasema, "Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu." Huyu "Yeye" ni nani? Neno la Uzima – Yesu!)
    3. Kama Mungu anasema kuna chaguzi mbili maishani, na Mungu yu bayana katika njia yenye nuru," je, hilo kimantiki halimaanishi kuwa kila amuzi linaangukia aidha kwenye uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya?
  3. Kujaribisha "Njia" Yako.
    1. Hebu tupitie upya. Yohana alianza kitabu chake (1 Yohana 1:1-4) kwa kusema kwamba alitutaka tuwe na ushirika na Mungu. Baadaye akatuambia kwamba maisha ni kama ujia/njia kwenye msitu mdogo/sehemu yenye miti mingi: Una nafasi ya kwenda kushoto au kulia. Ni njia moja pekee inayotuelekeza kuwa na ushirika na Mungu. Soma tena 1 Yohana 1:6. twawezaje kujua kama tupo kwenye njia sahihi? (Yohana anapendekeza "Kujijaribu mwenyewe.")
      1. "Jaribu" hili ni nini? (Kutembea gizani. Kama ukitembea gizani, haupo katika njia sahihi na hutokuwa na ushirika na Mungu.)
        1. Hebu subiri kidogo. Kuniuliza kama ninatembea "gizani" siyo ya msaada sana . Yohana anasema nini kutusaidia kujua kile inachomaanisha kutembea gizani? (Yohana anafafanua kwamba baadhi wanadai kwa uongo kuwa wanatembea nuruni. Unajaribisha hili kwa kuangalia kama wanaishi kwa kuifuata kweli.)
    2. Soma 1 Yohana 1: 8 & 10. Ni jaribu gani hili linalojaribisha kama tupo kwenye njia sahihi? ( Kama tutadai kuwa hatuna dhambi, tutakuwa katika njia potufu.)
      1. Je, hili ni jaribu la matendo yetu, kama katika 1 Yohana 1:6? (Hapana. Hili ni jaribu la mtizamo wetu, mafikara yetu. Badala ya kutumia neno "kudai" hebu tutumie neno "kufikiri" ili kulifanya liwe la binafsi zaidi.)
        1. Unafikiri huna dhambi?
        2. Kama utashindwa jaribu hili, matokeo yake ni nini? (Hatusemi ukweli. Hili linatuweka katika njia potofu – katika njia ya giza .)
        3. Unafikiri hawa watu wanajua kuwa wapo kwenye njia ya giza ? Kama mtu anadai kutokuwa na dhambi, ungedhani kuwa wasingekuwa watu "wema". (Baini tena maneno ya 1 Yohana 1:8. "Tunajidanganya." Watu hawa kwa hakika wanajidanganya kuhusu haki yao.)
      2. Ni katika mazingira yapi mtu au watu wangefikiri au kusema kuwa hawakuwa na dhambi? (Mtu ambaye angedai ukamilifu. Niliwahi kusikia binti mmoja aliyedai kuwa yeye ni nabii wa kisasa na pia kudai kwamba aliishi miezi sita iliyotangulia pasipo kutenda dhambi. Wale wanaodai kwamba tunaweza kuufikia ukamilifu katika matendo yetu wanatakiwa kutafakari fungu hili kwa makini sana.)
      3. Je, kuna mazingira mengine tena ambapo mtu anaweza kufikiri kuwa hakuwa na dhambi? (Kinyume cha hali ya ukamilifu ni kudai kwamba dhambi si dhambi tena kwa wenye haki. Hili ni wazo tunaloweza kulifanya tutakavyo, kwa sababu dhambi haihusiki tena kwa Wakristo. Dhambi haijalishi tena kwa sababu kwa namna fulani imebadilishwa katika haki. Yohana anasema kwamba dhambi ni dhambi na tunatakiwa kukiri/kukubali hilo.)
    3. Angalia tena 1 Yohana 1:10. Je, Mungu amekuwa akituongelea? Yohana anamaanisha nini pale anaposema kwamba madai kuhusu hulka/asili nzuri ya mwanadamu "humfanya [Mungu] kuwa mwongo?" (Mungu ametufunulia dhahiri hali halisi ya mioyo yetu. Katika Mwanzo 8:21 anatuambia kwamba kila "mawazo ya moyo [wetu] ni mabaya tangu ujana ujana." Katika Yeremia 17:9 anasema "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaje kuujua?")
    4. Soma tena 1 Yohana 1:8. Je, hatuna tatizo lingine? Wale walio katika njia sahihi, njia "nyepesi" wanawezaje kuwa wadhambi, wenye mienendo mibaya na kuwa waovu tangu ujana?
      1. Kama kwa Mungu hakuna giza kabisa, na tunatakiwa kuwa katika njia ya Mungu, twawezaje kuwa na dhambi ndani yetu?
      2. Unakumbuka swali langu pale mwanzoni kuhusu kama maamuzi yote maishani yalikuwa masuala "sahihi/makosa"? Twawezaje kuwa katika njia sahihi hali tukiendelea kuchagua dhambi? Je, hili siyo "jaribu" la kama tupo katika njia sahihi – kuishi kwa kufuata kweli (1 Yohana 1:6)?
  4. Asili ya Kutembea
    1. Kutatua hili tatizo la mwisho, hebu tuchukulie kwa makini neno "tembea." Ulinganisho wa Yohana ni kati ya kutembea nuruni na kutembea gizani. Unafikiri  inamaanisha nini "kutembea" nuruni au gizani? (Kutembea humaanisha kusogea. Vines hutufundisha kwamba wakati ambapo neno hili linamaanisha kutembea katika hali halisi katika sehemu nyingi kwenye Agano Jipya, kamwe haimaanishi kutembea katika hali halisi katika nyaraka za Yohana. Vincent's anaongezea kwamba Yohana anaongezea kuhusu "hali ya maisha iliyozoeleka ambayo ni ngumu kuiacha." Kutokana na hili ninaelewa Yohana husema kuwa "desturi yetu" ni kutenda uovu au wema.)
      1. Je, hili linatatua tatizo la kimantiki kuhusu jinsi ambavyo tunaweza kuwa katika njia nyepesi na bado tukiwa na dhambi katika maisha yetu? (Ndiyo. Dhambi ni kukengeuka/kupotoka kwa kuiacha njia, lakini lengo letu ni kuwa na mwelekeo wa jumla, desturi yetu maishani, kuishi kwa kuifuata kweli.)
      2. Hii inapendekeza nini kuhusu dhambi na kila maamuzi tunayoyafanya? (Maamuzi yanaweza yasihusishe dhambi, lakini yumkini inatuelekeza kuelekea au mbali na dhambi. Hili ndilo wazo la "kutembea." 
    2. Leo hii tatizo kubwa ni kuliita giza nuru. Tatizo hili ni kubwa kiasi gani katika muktadha wa mafundisho ya Yohana? (Hatuwezi kujua kuwa tupo katika njia potofu, hatuwezi kuenenda kuelekea kwenye barabara ya mabadiliko/matengenezo, isipokuwa tu tukikiri/kubali kuwa dhambi ni dhambi. Kama tutaiita dhambi kuwa haki, mara zote tutaendelea katika njia potofu hadi pale itakapotuua.)
  5. Njia Iliyofaulu
    1. Soma 1 Yohana 1:9. Wadhambi wanawezaje kuendelea katika njia nyepesi? Kama Mungu hana giza , sisi wanadamu tena tulio wadhambi twawezaje kufaulu kutembea katika njia nyepesi? (Mungu atasamehe dhambi zetu zilizoungamwa. Yesu anatufaulisha kwa ajili ya njia nyepesi!)
    2. Je, wale wanaotembea nuruni wana upeo wa uelewa wa dhambi zao? (Ndiyo. Hii inaelezea mjadala wa yesu kuhusu wale wanaodai (kimakosa) kwamba hawana dhambi. Mungu asifiwe kwamba kuna suluhisho! Tupo katika njia kuelekea kwenye ushirika hata kama tuna dhambi. Ukweli kwamba una dhambi maishani mwako hakukuondoi kuwepo kwenye njia "sahihi." Lakini, kumbuka kwamba kama unatembea gizani, haupo katika njia sahihi. Uelekeo wa maisha yako unahusika.)
    3. Je, hali ikoje kwako rafiki? Je, waziungama dhambi zako bila kusita? Au nawe unadai kutokuwa na dhambi? Upo katika njia kuelekea kuwa na ushirika na Mungu au katika njia kuelekea kwenye giza la milele?
  6. Wiki Ijayo: Kutembea Nuruni: Kutunza Amri Zake.

 

Wednesday, July 8, 2009

THE MOST IMPORTANT MEAL OF THE DAY

Breakfast is the most important meal of the day. Why? It is like taking an auto trip. If your gas tank is empty, when do you fill it up? Before you start the journey or when you arrive? Obviously, you need to be full of high octane fuel to begin your trip, otherwise you are headed for trouble. Likewise, think of your day as a journey; and think of your breakfast as providing energy to start that journey. You need more food energy at the beginning than at the end of the day.  

There is a lot of wisdom in the old saying, eat breakfast like a king, lunch like a prince and supper like a pauper.” In other words, breakfast should be just what the word implies: “breaking the fast” of the previous night.  One does not break a fast with more fasting.  Many Americans have it backwards—they skip breakfast, eat an inadequate lunch, and pack the majority of the day’s fuel supply into the evening meal.  However, this custom does not make good nutritional sense.

Check and balances exist to keep the level of our bodies’major fuel supply, blood glucose, within safe limits.  After a meal, any blood sugar that is not immediately needed is stashed away in muscles and the liver in a storage form called glycogen.  Liver glycogen serves to replenish blood sugar when needed.  During the night, liver glycogen kicks in and maintains a steady state of blood sugar for body needs.  But what happens when breakfast is skipped?  Problems can result, especially for the brain.  Without a proper supply of glucose, the brain doesn’t function well.  No wonder studies have shown that both children and adults do not perform at their best without breakfast.  

In spite of how important breakfast is, breakfast-skipping is all too common.  It is estimated that about 3 million American school-age children skip breakfast and have no school-breakfast program available to them.  About one in six teenagers goes to school without breakfast.  In a Michigan study, over 20 percent of freshman college students skipped breakfast.

Breakfast skipping is even more critical for children than for adults.  A greater drop in blood glucose can occur in children because their brain weight to liver-weight is proportionately greater.  This means that the liver will have proportionately less glycogen stores and thus be unable to maintain fating blood levels for as long as adults can.  In addition, since a child’s metabolism is greater, the brain’s demand for glucose will be proportionately greater than will an adult’s.  Obviously, the result could be a diminished brain function in children who skip breakfast, the bottom line: breakfast is important for providing brain fuel throughout the morning.

Another reason that breakfast-skipping combined with eating heavy evening meals is unwise involves the area of energy balance.  To be in energy balance means that the energy you take in as food and beverages is equal to the energy you expend.  When energy intake consistently exceeds energy expenditure, even by a small amount, the eventual result is extra pounds.  Keep in mind that typical evening activities are not real energy-burners: watching TV, reading, relaxing, talking with family and friends.  It certainly does not make sound nutritional sense to eat the largest meal late in the day when energy demands are reduced and the extra calories are easily converted into fat.

Breakfast should contain about one-third to one-half of the daily dietary needs.  Omitting breakfast can lead to vitamin and mineral deficiencies.  For example, a large percentage of preschoolers who skip breakfast fail to reach 70 percent of the Recommended Daily Allowances for many vitamins and minerals.  Other studies demonstrate that skipping breakfast results in substantial deficits in various essential nutrients among low-income children, and from older children and teenagers that are not from low-income families.  It appears that essential nutrients may not be adequately available if breakfast is not eaten on a regular basis.

The Iowa Breakfast Studies are frequently quoted to illustrate that hunger and under-nutrition have adverse affects on children’s learning ability.  They demonstrated that children consuming both breakfast and lunch at school are less likely to suffer from fatigue, irritability and an inability to concentrate.  If breakfast was eaten, work rate and output were improved as were the tasks performed later in the morning.

Later investigations, performed on 3 groups of Jamaican children, ascertained the effect of breakfast on various mental performance tests.  When breakfast was skipped, the nutritionally deprived groups cored lower on fluency, creativity and motivation, and scored lower in arithmetic and in visual short-term memory tests.  When compared with normal children, the undernourished children had poorer scores in arithmetic.  It appears that mental performance is more likely to be adversely affected in poorly nourished children who skipped breakfast.

What about well-nourished children?  Carefully controlled studies of well-nourished, middle-class children demonstrated that skipping breakfast has an adverse effect on a child’s late-morning problem-solving performance.  A significantly greater number of errors were made when breakfast was skipped.  Performance on an attention task and arithmetic of normal children with and without breakfast was measured at three different times throughout the morning.  Generally, children made more errors as the morning progressed, but at each time point, children having breakfast made fewer errors and were less variable in their performance.  Regarding the arithmetic task, eating breakfast made no difference in the early morning, but by mid-morning, those who ate breakfast exhibited a clear improvement over the skippers.  Apparently, brain function can be affected by subtle changes in nutritional status. 

Obesity continues to be a major problem in the United States.  While Americans are obsessed with eating fat-free foods, they continue to get fatter.  Interestingly, studies show that skipping breakfast is seen twice as commonly amongst obese children and adolescents than in those not obese.  Why is skipping breakfast associated with obesity?  Certainly, it increases the likelihood of snacking.  Snack, as we well know, are rarely carrot sticks or an apple, but are more often sugar-laden, high-fat convenience foods as chips, doughnuts, sweet rolls, candy, cookies and other junk food.

What about the breakfast habits and health of adults?  Two studies from California and Michigan found that men and women who regularly ate breakfast reported better-than-average health compared with those who skipped breakfast.  Furthermore, adults who ate breakfast had reduced levels of blood cholesterol, while breakfast skippers had elevate4d cholesterol levels. 

As mentioned earlier, breakfast should be king-size and hearty, providing from one-third to one-half of the day’s calories and protein needs.  Breakfast should typically be rich in carbohydrates, since glucose is the premium fuel for the brain and the body.  This means that one should eat liberally of whole grain, beans, fruits, and vegetables.  For example, one may choose to eat either steamed vegetables and brown rice, or whole grain waffles and fruit for breakfast.  The sugars found in fresh and dried fruits are wrapped in various dietary fibers, and contain an abundance of vitamins and minerals.

It is important that the starchy foods be whole grain, such as brown rice, whole wheat breads, waffles, bagels, muffins and pasta.  The unrefined grains are a wonderful source of vitamins and minerals, protein and fibers.  Dietary fiber plays an important role in helping to lower blood cholesterol levels, promote regularity, and help protect against colon cancer.

For good health it is important to choose foods for breakfast that are rich in vitamins and minerals and low in fat, saturated fat and cholesterol, yet high in satisfaction.  Egg, bacon, sausage, and omelettes and loaded with artery clogging saturated fat and cholesterol.  Pancakes, waffles and French toast that are made with milk and eggs and then freely served with butter or cream are likewise unhealthy for the heart.

Another category of breakfasts that are not the most healthful are those loaded with sugar.  Sweet rolls and pastries, doughnuts, pies, sweet cakes, and sugar-loaded cereals all pamper the sweet tooth.  Besides being sugar-laden, such items are usually made with white flour and generous amounts of fat.  Both the sugar and the white flour have been robbed of many minerals and vitamins during the refining process.  A large ingestion of sugar at one time can produce a sharp rise in blood sugar levels.  This, in turn, is flowed by a sharp decline in blood glucose due to an insulin surge.  The hypoglycemic reaction causes feelings of hunger.  A situation that provides no staying power but rather a “roller coaster” blood sugar swing.

Eating a good breakfast is supportive of good health.  Skipping breakfast is associated with mid-morning fatigue, sluggish mental achievement, and a greater risk of accidents.  The benefits of regularly eating breakfast are best appreciated by experience.  A good breakfast is an essential part of our daily routine—the best meal of the day.
 

Monday, July 6, 2009

SOMO LA 2: KUPATA UZOEFU WA NENO LA MUNGU

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N.Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.

Utangulizi: Nipo Kalifornia kwa sasa. Kwa miaka mingi niliyokuwa nikitembelea Kalifornia nimejifunza kwamba sehemu kubwa ya wakazi wake hupenda kuonekana wadogo. Kundi hili linakinzana na mfumo wa asili wa maisha ambapo umri mkubwa hutamaniwa kwa kuwahuleta busara na heshima. Badala yake, kila mtu hutaka kuonekana mdogo milele. Kwa nini iko hivi? Nafikiri sehemu kubwa ya sababu ni kuwa ujana ni sawa na maisha yenye msisimko. Utu uzima wenyewe nao ni sawa na kifo. Ujana na maisha ni mambo ya kusisimua na yenye mvuto. Kifo kwa kweli chenyewe huchukiza. Somo letu wiki hii linapendekeza njia nyingine ya maisha (na ujana. Je wewe ni mtu atakaye kuwa kijana milele? Unatamani furaha ya maisha? Basi na tuzame katiaka somo letu na tuona zaidi juu ya maisha ya milele na ujana.

I. Shuhuda wa Maisha

A. Tusome 1 Yohana 1:2. Wiki iliyopita tulijadili kauli ya Yohana ya kwamba Yesu ni “neno” la uzima. Sasa Yohana anasisitiza sehemu ya pili ya sentensi “uzima.” Ni nini kilicho muhimu katika kumuita Yesu “Uzima” wakati tayari tumeshamwita “Neno?”

1. Je umewahi kusikia mtu akizungumzia mada na ukahitimisha ya kuwa hawafahamu wanachozungumzia? (Yohana anatuambia ya kwamaba Yesu siyo tu kwamba anatupa maelekezo kuhusu maisha (“Neno”), bali Yesu ni uzima.)

2. Ni kwa jinsi gani Yesu ni “Uzima?” (Wiki iliyopita tulijifunza kwamba Yesu ni muumba wetu, hii humfanya yeye kuwa asili ya uzima. Yohana anashuhudia ya kwamba Yesu alifufuka nay a kwamba yu hai. Hii inaonyesha kwamba Yesu anao uzima sasa. Ufufuo unaonyesha nguvu ya “uzima” hata katika nyakati ambapo kifo kimetokea.

B. Wakati Yohana akiandika katika 1 Yohana 1:2 kwamaba “uzima huo ulipodhihirika” ni hoja gani anayojaribu kuijenga? Mara mbili ametumia neno “kudhihirika.” Je ungeweza kusema (juu ya mtu mwingine) ya kwamba “wanadhihirika” (Hapana. Mungu hudhihirika kwa wanadamu. Yohana anatuambia kwamba Mungu alifanyika mwili na kasha Mungu akaungana na wanadamu wengine. “Uhai huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu..” Kiini ni katika Mungu kushuka chini na kudhihirika kwa wanadamu.)

1. Je Yohana anafundidha nini juu ya uhusiano wa Yesu na Baba Mbinguni? (Yohana hajengi utata katika hili. Anasema kwamba Yesu alikuwa na Mungu na kisha akatokea kama mwanadamu. Yesu alikuwa na asili yake mbinguni. Aidha uliamini hili au usiliamini. Hauwezi tu kwa mantiki, kama baadhi ya viongozi wa kidini na watu wengine, uamini ya kwamba Yesu alikuwa tu ni rabbi mwenye busara au mtu mzuri.kufanya hivyo kunamfanya Yesu na wale wote waliokuwa wasshriki wake kuwa ni waongo wenye kufedhehesha. Aidha ukubali imani itawale au ukatae. Hakuna msimamo wa kati katika hili.)

C. Soma 1 Yohana 1:3. Je ni kauli gani nyingine tena aletayo Yohana juuu ya Yesu? (Anatuambia ya kwamba mbali na asili ya Yesu kuwa mbinguni, Yesu ni “Mwana” wa Mungu. Anatoa taswira ya ulimwengu kwa kuita sehemu moja kuwa “Father” na nyingine “Mwana”)

1. Hii si mada ya juujuu. Soma Kumb. 6:4. Hili lilikuwa mojawapo ya fungu la muhimu sana kwenye Biblia kwa mujibu wa wachambuzi wa kiyahudi wa nyakati za Yohana. Tunatatuaje hili jambo na taswira ya Yesu kuwa mwana wa Mungu? Yesu anawezaje kuwa Mungu, wakati kuna Mungu mmoja tu?

a. Tafakari kidogo katika fungu hili la Kumb 6:4. Utawezaje andika hili isipokuwa Mungu wako ana Nyanja? (Nafikiri hii inasisitiza dhana ya Utatu, wazo ya kwamba Yesu na Mungu Baba ni Mungu mmoja.)

2. Soma Mwanzo 1:1-2. Neno la kkiebrania “Mungu” katiak aya ya kwanza ni neno la wingi. Je hii hutufundisja nini juu ya Utattu? (Katika injili yake na nyaraka zake Yohana anaanza uandika kama kitabu cha Mwanzo. Ni katika kitabu cha Mwanzo tunaona dhana ya Mungu kuonyesha Utatu. Yohana anaelezea ya kwamba utatu huu unamjumuisha Yesu kama Mwana na Muumba.)

II. Shuhuda wa Upendo

A. Tazama tena katika 1 Yohana 1:3. Ni kwanini Yohana anasema anatoa ushuhuda wake juu ya Yesu? Ni nini nia yake? (ili wasomaji wake wa waweze kuwa na shirika naye.)

1. Yohana ameshafariki. Twataabikia nini? Ni aina gani ya shirika aliyo nayo Yohana? (Yohana anasema ushirika wake hakika ni wa pekee. Yohana anafanya shirika na “Ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na mwana wake Yesu kristo.)

B. Zingatia yaliyomo katika ushuhuda wa Yohana katika 1 Yohana 1:3. Anaunganisha “ushirika” na kile alichokiona na kukisikia. Ni kwa jinsi gani hiyo inatusaidia kuwa na shirika na Mungu Baba na Mungu Mwana, Yesu? (Kama tusipoelewa asili ya Mungu na ya kwamba Yesu ni Mungu, hatuwezi kuwa na shirika na Mungu.)

1. Hata hivyo, kuwa na shirika ni nini, hata tutamani hivyo? (Kuwa shirika ni kumfahamu mtu, kuwa na muda naye wa pamoja. Yohana anasema, “tazama nimekuwa na muda na Yesu. Namfahamu. Endapo kama utatumia muda wako na ujumbe huu, utakuwa “unatumia muda” wako ukiwa na Yesu na utamfahamu.”)

a. Je unafurahia kusoma kitabu hiki? Kuwa na fursa ya kumjua Yesu na kuwa na shirika na Mungu?

C. Soma Yohana 14:7-9. Yesu anasema kuwa tukimjua yeye, tumemju aBaba. Je Yohana anaelezea zaidi kauli ya Yesu? (Yesu ni Mungu na shahidi wa mambo ya mbinguni. Yohana ni shahidi wa Yesu. Tuna mtiririko wa kuaminika wa taarifa.

D. Soma 1 Yohana 1:4. Je kauli hii si kwamba ingesema ya kwamba Yohana anatuandikia ili kutimiza furaha yetu badala ya kutimiza na furaha yake pia? Hata hivyo, yeye tayari anamjua Yesu. Yeye tayari yupo kwenye hili kundi malum lenye shirika na Yesu.

1. Hebu fikiria mtu akwambie kwamba atakupeleka ikulu ya Marekani (tena pasi gharama) na kukutambulisha kwa rais wa Marekani. Je haitokuwa bayana ya kwamba lengo lilikuwa kufanya siku yako kuwa njema badala ya kufanya siku ya mheshimiwa rais njema?

2. Hebu jenga picha ya taswira na fikiria ya kwamba umepelekwa kwenye klabu ya Muumba na Bwana wa ulimwengu. Je hi ni kwa manufaa yako au yake?

3. Ni kwanini Yohana ana mtizamo huu wenye kuonekana kinyume? (Kitu kisicho cha kawaida na muhimu sana kinasemwa hapa: Mungu anataka ushirika na wewe. Inampa Mungu furaha kuwa na shirika na sisi!)

E. Soma Yohana 15:15. Ni uhusiano wa aina gani ambao Mungu anataka kuwa nao nasi? Je ni wazo gani yeye mwenye uzima wa milele analo juu yetu? ( Yesu anatuita sisi “rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.” Fungu linalofuata linaendelea kwa kusema kwamba Yesu alituchagua sisi, hatukumchagua yeye. Alitutaka sisi ali tuweze kuwa naye kwake!)

1. Je huleta hisia gani kuwa rafiki wa Mungu?
2. Je waweza tumia furaha zaidi katika maisha yako?
3. Dhambi ina raha zake, ama la hakuna ambaye angafanya dhambi. Kama una uzoefu na dhambi nzito, je waweza shuhudia ya kwamba utii kwa Mungu huleta furaha halisi na ya kudumu?

a. Hebu fikiria uzoefu wa Gavana wa Kalifornia Kusini (ambaye majuzi alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa wa muda mrefu). Kama angekuwa na fursa ya kuandika tena historia yake katika kiaka michache iliyopita, je unafikiri angefanya nini? (Kwa wasomaji wasiofahamu Gavana amefedheheshwa sana, angeweza kupoteza familia yake na amepoteza sifa ya kuwa makamu wa rais wa Marekani kwa sababu alijihusisha na uhusuano wa kimapenzi na mwanamke mmoja wa Argentina.) Je, unafikiri ana furaha sasa?

F. Katika 1 Yohana 1:4 Yohana anajijumuisha katika “furaha yetu.” Pale tuletapo wengine katika kundi hili la wenye urafiki na Mungu, je huleta furaha?

G. Rafiki ungependa kuwa rafiki wa Mungu? Je, ungependa kuingia katika jamii yenye nguvu kabisa ya mawiliki katika ulimwengu? Ungependa furaha ya kudumu? Kama ndivyo, wiki ijayo na tuedelee na safari yetu ya kusoma na kujifunza zaidi juu ya ujumbe wa Yohana kwetu.

III. Wiki ijayo: Kutembea Nuruni: Kugeuka na Kuiacha Dhambi