(Kutoka 20, Mathayo 5, Wakolosai 2, Waebrania 4)
Maisha ya Mkristo: Somo la 8
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.
Utangulizi: Kama kuna kitu kinahitajika kufanyika, nataka kukifanya sasa hivi. Kama una furaha kama mimi, basi pumziko la "uhuru wa hatia" ni la thamani kubwa. Hiyo ndiyo maana ninaipenda sana Sabato. Nafahamu kwamba sitakiwi kufanya kazi siku ya Sabato, kwa hiyo naweza kupumzika pasipo kujisikia hatia. Wakati nikiwa katika mafunzo ya uanasheria, kilikuwa kipindi kizuri sana. Marafiki zangu wa dhati walikuwa wakisoma kila siku ili waweze kupata alama nzuri na kufaulu kwa madaraja ya juu. Sikusoma sheria siku ya Sabato na nilibarikiwa kwa hilo. Hebu tujivinjari ndani ya Biblia ili tuweze kubaini kuwa kwa nini pumziko la Sabato bado ni sehemu muhimu ya mpango wa Mungu kwa ajili yetu!
I. Madhumini ya Sabato
A. Soma Kutoka 20:8-11. Mungu anatoa sababu gani kwa ajili ya kuitunza Sabato? (Kwa kukumbuka ukweli kwamba aliziumba mbingu na nchi.)
- Soma Mwanzo 2:2-3. Pale Mungu alipoumba Sabato kwanza, kusudi lake lilikuwa ni nini? (Sababu ile ile iliyoelezewa katika kitabu cha Kutoka-kwa sababu aliuumba ulimwengu.)
C. Hebu jaribu kujiweka katika nafasi ya Mungu. Mara kwa mara huwa tunasema ya kwamba kwa nini sisi, kama wanadamu, tumfuate Mungu. Ni nini mtazamo wa Mungu juu ya hili? Kama ungekuwa Mungu na uulizwe ya kwamba kwa nini wanadamu wakutumikie, ungesemaje? (Kwa sababu Niliwaumba!)
1. Je, hiki ndicho kwa hakika ambacho Mungu anakisema? (Soma Mwanzo 1:1. Hili ndilo tamko la Mungu la kwanza kwetu-ya kwamba yeye ni Muumba.)
- Soma Ufunuo 14:6-7. Tumeangalia madai ya Mungu ya kuabudu katika kitabu cha kwanza cha Biblia. Mungu anatoa sababu gani katika kitabu cha mwisho cha Biblia? (Sababu ya kumwabudu Mungu ni kwa sababu yeye ni Muumba wetu. Kwa hakika, hii inaitwa "injili ya milele".)
- Orodha ya Naves namba 104 mafungu ya Biblia chini ya "Muumba," ambapo Mungu aidha moja kwa moja au kupitia kwa wanadamu, anaweka dau madai yake kwa mamlaka juu ya wanadamu katika ukweli wa Uumbaji wake.)
- Muda wa mkakati. Kama ungekuwa Shetani, na ungekuwa katika shindano na Mungu juu ya mamlaka kwa wanadamu, lengo lako lingekuwa nini? (Kuhafifisha au kondoa kabisa msingi wa madai ya Mungu ya mamlaka.)
- Je, tunaona hili likitokea: je, historia na ukumbusho wa madai ya Mungu ya mamlaka yamemomonyolewa?
- Je, mmomonyoko huu wapaswa kuwa na maana yoyote kwa Wakristo? (Martin Luther alisema: " Kama nikitamka kwa sauti kubwa kabisa … kila sehemu ya Neno la Mungu isipokuwa kwa usahihi kwamba sehemu ndogo ambayo dunia na mwovu wanashambulia kwa wakati huo, simkiri Kristo….pale ambapo pambano linapopamba moto, hapo ndipo uaminifu wa askari unajaribiwa.")
- Wengi wanasema kuwa Sabato si ya maana tena. Kama Martin Luther yuko sahihi, je, Sabato haipo katikati ya pambano kati ya Yesu na Mwovu?
- Kama ipo katikati, je, "tunamkiri Kristo" kama tunashindwa kuchukua msimamo thabiti kwa kukumbuka mamlaka ya Mungu kwa wanadamu kila wiki?
Sabato, Bado ni Sehemu ya Mpango wa Mungu?
- Wiki iliyopita tulijadili juu ya "Neema," na kugundua (Warumi 8:2) kwamba "sheria ya Roho wa uzima imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na mauti." Je, hiyo inamaanisha kuwa Amri Kumi (ikijumuisha amri ya Sabato) zimekufa?
- Soma Mathayo 5:17-19. Yesu anasema nini katika lengo lake la kuja duniani? (Siyo kufuta/kukomesha Amri Kumi! Bali , alikuja "kuzitimiliza." Lazima nisiwafundishe wengine kuzivunja amri.)
- Je, hiyo inamaanisha nini-kutimiliza? (Tulijifunza wiki iliyopita kwamba Yesu alikuja na kufaulu pale ambapo Adamu alishindwa-katika kutunza sheria za Mungu. Lakini, tulijifunza pia kuwa hii siyo leseni (Warumi 6:1) ya kutenda dhambi na kwamba tunatakiwa kuishi maisha "kwa mujibu wa Roho." Warumi 8:5. Hili liko sawa na kauli ya Yesu kwamba kamwe tusimfundishe mtu yeyote kuvunja amri.)
- Soma Wakolosai 2:16-17. Hadi hapa tumeshaona kwamba Sabato ipo katikati ya mkwaruzano/ugomvi/pambano na Shetani kwa sababu ni kielelezo cha mamlaka ya Mungu kama Muumba wetu. Je, hapa Paulo anasema kwamba Sabato si kitu? Je, Paulo atakuwa "mdogo" katika ufalme wa mbinguni? (Paulo anaonekana kunukuu kwa harakaharaka kutoka katika kitabu cha Hosea 2:11. Hapo, marejeo ni kwa sikukuu za Kiyahudi ambazo pia ziliitwa kuwa "Sabato." Kwa hakika, neno la Kiyunani liitwalo "Sabato" katika Wakolosai 2:16 ni wingi kwa hakika: "Sabato." Tafsiri nyingi (lakini siyo ya New International Version) zinatafsiri neno "Sabato.")
- Paulo anamaanisha nini kwa kuziita Sabato "kivuli cha mambo yajayo?" (Tangu Yesu atimilize huduma za patakatifu za Agano la Kale,inafuata kimantiki kwamba sikukuu za Sabato za Wayahudi, ambazo zilikuwa sehemu ya mfumo wa kafara, zilitimilizwa. Hii haikuwa kweli kwa Sabato ya kila wiki ambayo ilikuwa ukumbusho wa uumbaji, na siyo sehemu ya huduma za patakatifu.)
- Wachambuzi wengi wa Biblia, hususan wale wa kale, wanakubaliana na hoja yangu kwamba Wakolosai 2 hairejei Sabato ya kila wiki. Chukulia kile ambacho nukuu za Barners zinasema kuhusu fungu hili (na hili ni mfano hasa wa mengine). Kwanza anatabanaisha kuwa neno hilo ni wingi na kwa hiyo inarejea kwenye sikukuu za Kiyahudi, halafu anaendelea: "Hakuna sehemu ya sheria ya maadili-hakuna hata moja ya amri kumi ingeweza kuongelewa kama 'kivuli cha mambo yajayo.' Kutokana na asili ya sheria za maadili, amri hizi zinawajibika milele na kila mahali.")
- Soma Waebrania 4:8-11. Miaka ya hivi karibuni baadhi ya watu wameanza kujenga hoja kuwa tangu ufufuo tumeingia katika wakati wa "Sabato." Kila siku ni Sabato. Ni nini ambacho kingekuwa matokeo ya kimantiki ya hiyo hoja? (Aidha usingeabudu katika siku yoyote au ungeabudu katika siku yoyote.)
- Kitabu cha Waebrania kinapendekeza nini kuhusu muda wa kawaida wa kukutana kumwabudu Mungu? (Soma Waebrania 10:25. Inatuambia kuwa yatupasa kukutana pamoja mara kwa mara.)
- Kama ungekuwa unasheherekea kuishi katika "wakati wa Sabato," na ukafikiria kuwa unapaswa kukutana mara kwa mara kumwabudu Muumba wako, ni siku ipi ambayo kimantiki ungeichagua? (Soma tena Waebrania 4:9-10. Kama sisi ni wa kuingia katika pumziko la Mungu, kama jinsi Mungu alivyofanya, tungeabudu siku ya Jumamosi! Hili ndilo hitimisho la pekee linaloleta mantiki.)
- Wengine wanajenga hoja, ambayo haijengwi kwenye amri yoyote kutoka kwa Mungu inayopatikana kwenye Biblia, kwamba ufufuo wa Yesu siku ya Jumapili ulibadilisha kila kitu kuhusu Sabato. Je, wafuasi wa Yesu wana sababu yoyote ya kufikiri kwamba hiyo ni kweli?
- Yesu alisulubiwa siku gani? (Soma Marko 15:42-44. Ijumaa.)
- Soma Mathayo 27:50-52. Je, kuna sababu yoyote kwa nini Yesu asingefufuka papo hapo, na katika ushuhuda wa macho ya waliokuwepo ajitoe msalabani kwa kutumia uwezo mkubwa kabisa na utukufu uwe kwa Baba yake?
- Wewe, ukiwa kama mzazi, ukimwona mwanao akiteswa na kupigwa, je, usingetaka kumwokoa mara moja?
- Wewe, ukiwa kama mzazi, ukimwona mwanao akishinda mpambano wa muhimu sana ulimwenguni, ungependa kusubiri kidogo, tena si siku nzima kumkumbatia kwa kumpongeza na kumpa hongera?
- Kwa nini Yesu alisubiri? Dhidi ya silika zote za asili, kwa nini Yesu na Baba walisubiri? (Yesu alipumzika siku ya Sabato kwa sababu ile ile aliyopumzika siku ya Sabato baada ya kuumba ulimwengu. Alikuwa anakumbukia kazi yake halisi/ya awali ya uumbaji na sasa kazi yake ya mwisho kabisa ya kuuokoa uumbaji wake dhidi ya uharibifu.)
Kuitunza Sabato
- Kwa mwangaza wa historia ya msingi wake, ni kwa jinsi gani utaitunza Sabato? (Ni siku ya kuachana na kazi na mambo yote ya dunia na kumsheherekea Muumba na Mkombozi wetu! Ni siku maalum ya kusifu na kuabudu.)
- Soma Marko 2:23-28. Je, hapa Yesu anasema kwamba kwa kuwa Daudi alivunja sheria ya mkate iliyowekwa wakfu, wanafunzi wake wanaweza kuvunja sheria ya usifanye kazi siku ya Sabato? (Hapana. Yesu anasema kwamba Sabato ilikusudiwa kwa ajili ya matumizi mazuri ya mwanadamu. Mbaraka wa wanadamu, siyo sheria na kanuni zisizo na msingi/sizizo na umuhimu, ndio madhumuni/makusudi ya kufaa ya Sabato.)
- Rafiki, unasimama wapi katika pambano dhidi ya mamlaka ya Mungu? Je, u askari mwaminifu na mtiifu kwenye masuala yenye mabishano? Kama siyo, unakosa mojawapo ya mibaraka mikubwa ya Mungu kwa ajili ya wanadamu! Kwa nini usidhamirie sasa hivi kuwa mwaminifu na ubarikiwe pale linapokuja suala la Sabato?
Wiki Ijayo: Mbingu.
No comments:
Post a Comment