Vijana waliokuwa wanachama wa chama cha wanafunzi wa Kisabato katika vyuo walifanya huduma ya kwenda kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Kisarawe iliyopo mkoa wa pwani. Katika programu hiyo iliyoitwa "Huduma yangu kwa Yesu" zaidi ya watu thelathini na mbili (32) walishiriki. Huduma hiyo ilianza kwa wana na binti za Mungu kusali na kupata fursa ya kuhudumu katika kanisa la Kisarawe na ndipo mchana wakaenda hospitali.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo
Wakati wa mjadala wa lesoni kanisa la wasabato Kisarawe
Maandalizi kwa ajili ya huduma kuu, kutoka kulia, Enos Manusu, James Sanawa, Rubara Marando na Bambino Philips
Muimbishaji, Nelson Nyahonyo akiongoza wimbo wakati wa huduma kuu
Kikundi cha uimbaji cha ZION MELODY kikiimba wakati wa ibada
Kusabahiana baada ya huduma
Kusabahiana kwa kukumbatiana miongoni mwa wasafiri wa mbinguni
Wana ASSA na wana THISDASO wa zamani wakiwa pamoja
Kutangaziwa utaratibu mzima utakaofuata kuelekea "huduma yangu kwa Yesu"
Kabla ya kwenda hospitali thisdas_sociates walikabidhi vitu kwa ajili ya kapu la DORCAS baada ya ibada
Muda wa kuhudumia hekalu la Bwana
Watu wa Mungu wakitumia
Watumishi wakipanga vitu kupeleka kwa wasioweza katika hospitali ya Kisarawe
Watumishi hawakutoa vinyonge bali walijinyima kwa ajili ya ndugu zao
Wajoli wakiingia wodini tayari kuwatendea miongoni mwa wale walio wadogo
Mgonjwa akifarijiwa na dada Neema Opiyo
Mrs. Tang'are aitwaye Jessie na Naphtali wakiwapa faraja wagonjwa
Katika kila wodi baada ya kuongea na wagonjwa na kuwapa faraja basi tulipata muda wa kuwaombea.
Heart to heart (this is my favorite picture)
Daktari mkuu Mr. Ogha akiongea na wageni kuwashukuru kwa huduma yao ya kuwatembelea
Viongozi wa kamati yetu ya programu kuanzia kushoto ni mwenyekiti ndugu Enos Manusu na ndugu Bambino Philip
Kijana Eliya wa Minaki akiaga kwa niaba ya wenzake baada ya huduma
Kundi zima la waliohudumu siku hiyo wana thisdas_sociates, isipokuwa Mgune Masatu (mpiga picha,)washiriki wa kanisa la Kisarawe,Mganga mkuu na wana ASSA wa Minaki sekondari.
Mpiga picha wetu ndugu Mgune Masatu
Shukrani kwa wana thisdas_sociates kwa kuandaa tukio hilo zuri kwa watu wa Bwana kwenda kutoa huduma katika jamii, shukrani pia kwa mzee wa kanisa la Kisarawe mzee Clauds na kanisa zima kwa ujumla kwa kutupa ushirikiano katika uendeshaji wa zoezi zima, shukrani kwa mamlaka za hospitali zilizotufungulia mikono na kutuwezesha kuwafikia wenzetu,shukrni kwa wanafunzi wa MInaki sekondari, shukrani pia kwa mtu mmojammoja ambaye alijikana nafsi kwa namna moja ama nyingine ili kuliinua jina la Bwana na mwisho shukrani kwa Mungu wetu wa mbinguni aliye mmiliki wa vyote na aliyetupa vyote tuvitumie kwa utukufu wake. Bwana atubariki tunavyozidi kutafakari kuwatendea miongoni mwa wale walio wadogo.
Nice presentation mzee.
ReplyDeleteThis shows Engineer can fit even in media. Big up.
Also congts and may GOD bless you for that brother.
Be blessed you brotheren.
Senzia Warema
The weaker one
SAFI SANA. MZINDI KUMTUMIKIA MUNGU. "Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana." 1 corinthians 15:58
ReplyDeleteBwana awaongezee mara zote mnapohitaji ili kutimiza matakwa ya Yeye aliye-wapeleka. Mungu awabariki
ReplyDeletengoja niandike kwa herufi kubwa.
ReplyDeleteKWELI HII NI SAFARI. SIYO YA KWENDA MWANZA AU LONDON BALI YA KWENDA MBINGUNI. NDIVYO YESU ALIVYOTUFUNDISHA.
I HAVE NO WORD WHICH CAN FIT MY APPRECIATION TOWARDS WHAT YOU HAVE DONE.
MAY BE LET ME SAY GOD BLESS YOU ABUNDANTLY, NEVER STOP DOING THAT AND OTHER SIMILAR 'HUDUMA YANGU KWA YESU' TEACH AND ENCOURAGE OTHERS YOUNG AND OLD WHENEVER YOU GO.
BUT REMEMBER TO TEACH TOUR CHILDREN TO GROW IN THE SAME TRACK.
MUNGU AWABARIKI SANA.
yes THAT IS GOOD
ReplyDeleteREMEMBER, REMEMBER TO TEACH TOUR CHILDREN TO GROW IN THE SAME TRACK.
mgataema@yahoo.com
Hii ndiyo dini ya kweli
ReplyDelete