Hesabu 5 & 6: Somo la 2
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.
Utangulizi: Wasomaji wasio na uzoefu wa Agano la Kale wanaweza kuudhika/kughafilika pale wanaposoma sura mbili za kitabu cha Hesabu ambacho tunazisoma hivi leo. Kwa kuwa sisi siyo walengwa, wala hatupo katika mazingira yao (kundi kubwa likisafiri kwenye jangwa la kutisha), siyo sehemu ya mfumo wa hekalu, waweza kuuliza “Kuna haja gani kwanza tujifunze haya?” Wakristo wengi wanaamini kwamba kile kilichoandikwa kwenye Biblia kina ushauri usio na kikomo wa vizazi vyote vya wafuasi wa Mungu. Kuna kanuni (na huenda zaidi) katika kitabu cha Hesabu zinazoendelea kutufundisha kuhusu njia za Mungu na mipango yake na matarajio yake kwetu. Hebu tuzame kwenye somo hili la kuvutia!
I. Matengenezo ya Kiafya
A. Soma Hesabu 5:1-3. Je, hivi ndivyo ambavyo ungemtendea mgonjwa?
1. Je, watu wote walioelezewa hapa ni wagonjwa? (Hapana. Wengine ni “najisi kimapokeo ama kutokana na taratibu tu.")
2. Kama si kila mmoja aliyetolewa ni mgonjwa, je, hili linaleta mantiki gani kwetu hivi leo? (Mtu aliyefariki aweza asiwe amekufa kutokana na uzee. Kwa vile mtu aliye “najisi” amegusa maiti, wanaweza pia kuwa wametwaa baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukiza.)
3. Unapotafakari hizi kanuni, je, ni kwa ajili ya manufaa ya watu au la? Je, zina huruma au la? (Pamoja na hawa watu wote wanaosafiri katika hali ya mawasiliano ya ukaribu, kuwatenga wagonjwa (na wale wanaoweza kuambukiza wengine) hadi pale wanapopona, au wanapothibitishwa kuwa hawana magonjwa tena, ni mbaraka mkubwa kwa wote waliosalia.)
B. Angalia tena Hesabu 5:3. Kwa nini Mungu anapendekeza kuwa kanuni hii inahusika naye na si afya za watu? (Mungu ndiye mmiliki wa watu hawa. Ni wake yeye. Anataka kambi lenye afya kwa ajili ya watu wake. Inatukumbusha juu ya asili takatifu ya Mungu.)
1. Tunajifunza somo gani hapa tunapofikiri kwamba Mungu “anadhibiti uhuru wetu” na kanuni zake za kiholela au zisizo na msingi? (Mungu kwa uhakika anatutafuta. Tunaweza kufikiri kwamba kanuni zake ni za kiholela, lakini anatujali na kututhamini mawazoni mwake.)
C. Soma Hesabu 5:4. Unafikiri hawa watumwa walioachiwa hivi punde wanaelewa kwa nini Mungu aliweka hivi vigezo? (Inawezekana hawakuelewa sababu, lakini habari njema ni kwamba walitii.)
II. Mageuzi ya Kisheria
A. Soma Hesabu 5:5-7. Nini lalamiko lako kubwa kuhusu mfumo wa sheria za makosa ya jinai? (Nchini Marekani, lalamiko moja kubwa ni kwamba kama anazo, basi mwathirika ana haki chache. Mara chache sana mwathirika anafidiwa kwa madhara aliyoyapata.)
1. Biblia inapendekeza adhabu gani? (Kwamba mwathirika si tu ana haki ya kufidiwa kikamilifu, lakini pia malipo ya ziada ya 20% kwa athari alizozipata.)
2. Nchini Marekani, kwa ujumla mwenye hatia anafungwa gerezani. Mfumo upi ni bora? Mfumo wa Biblia au mfumo wa Marekani? Idadi (nayo ni kubwa) ya wafungwa inahusisha wakosaji wasio na vurugu. Walipa kodi hugharimika – kuwalisha, kuwalaza na kuwavisha watu waliomo magerezani. Mfumo wa Marekani huhitaji fedha nyingi-fedha zinazotoka kwa watu wasio na hatia na ambazo hazielekezwi kuwasaidia waathirika wasio na hatia. Vilevile, haionekani kuwasaidi sana wenye hatia isipokuwa kuwafungilia mbali nasi)
B. Ona jinsi Hesabu 5:6 inasema kuwa mtenda dhambi “siyo mwaminifu kwa Bwana.” Hili lina ukweli gani? Je, mtenda dhambi siyo mwaminifu kwa mhanga? (Hawa sasa ndiyo waliokuwa watu wa Mungu pamoja naye safarini. Aliwaumba yeye, hivyo kushindwa kokote kuishi kutokana na viwango vyake ni kumkosea yeye)
1. Je, kuna dhana yoyote hafifu kama hii hivi leo? (Nina uzoefu na mfumo wa jinai wa Marekani tu, nao ni kama huu kabisa. Yaani ukivunja sheria, lalamiko la jinai huletwa katika jina la Jamhuri. Mamlaka kuu inasema, “Hizi sheria ni zangu ili kuwalinda watu, nanyi mmetenda kinyume dhidi yangu. Hivyo umenikosea mimi.” (yaani jamhuri inamtangazia mhalifu kwamba mhalifu ameikosea jamhuri kwa kuhalifu sheria zake za kuwalinda watu wake yeye Jamhuri).
2. Hesabu 5:7 inasema kuwa mtu lazima aungame. Ungamo linafanywa kwa nani? (Fungu linasema kuwa “dhambi” inaungamwa-na hiyo ni kwa Mungu. Kuna vitu viwili vinaendelea hapa: Kwanza, adhabu ya 20% husawazisha mambo na mtu aliyetendewa kosa. Pili, ungamo husawazisha mambo na Mungu.)
III. Matengenezo ya Ndoa
A. Pitia kwa haraka haraka Hesabu 5:11-28 na usome Hesabu 5:29-30. Una dukuduku gani na huu mwenendo/utaratibu? (Ni kwa nini kwamba mwanamke, na siyo mwanaume, ndiye anapaswa kupitia haya yote? Kwa nini wivu tu ndiyo ujenge huu utaratibu? Wivu waweza kuwa dhambi-na ndiyo ulikuwa msingi kwa mauaji ya kwanza kabisa, sawa? (Mwanzo 4))
1. Je, hii ni adhabu ya kawaida ya uzinzi? (Soma Mambo ya Walawi 20:10. Hii siyo adhabu ya kawaida. Adhabu ya kawaida ni kwamba mwanamke na mwanaume wote waliofanya uzinzi watauawa.
2. Soma Kumbukumbu la Torati 17:6. Ni nini kilichokuwa kinakosekana kwenye “utaratibu wa wivu” wa Hesabu 5? (Hakuna mashahidi. Walihitajika mashahidi wawili au watatu ili kutekeleza adhabu ya kifo katika Mambo ya Walawi 20:10.) concerns
3. Fikiria kwa muda mfupi tu na uweke pembeni mtazamo wako wa kileo/kisasa kuhusu usawa.(wa jinsia) Ni tatizo la aina gani katika aina ya familia iliyoelezewa hapa? (Mashitaka kati ya mume na mke. Ndoa inavunjika. Mahusiano yanaharibiwa yakiwa yamejengwa kwenye mashaka yanayoweza kuwa ya kweli au si ya kweli.)
a. Mpango wa Mungu unatimiza nini? Lengo gani linatoshelezwa na huu utaratibu? (Inaleta mwisho wa wivu na mashaka. Ama Mungu anamdhihirisha mke kuwa hana hatia (ni nani awezaye kubishana na Mungu?), au mke anafariki. Wachambuzi wa Kiyahudi wanasema kwamba mwanamke angeweza kukataa kula kiapo, angeungama, na kutalikiwa tu. Hakuna kifo kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha.)
B. Kuna somo gani kwa ajili yetu leo hii? (Vingi ya tuvionavyo kwenye luninga na kwenye sinema hutukuza uzinzi. Uzinzi ni tatizo la kutisha katika jamii na hata kanisani. Ujumbe/Hoja ya Mungu katika hili ni wa namna mbili: Anachukia uzinzi na anataka kuleta amani kwenye ndoa ambazo tuhuma kama hizi zimeibuliwa. Mungu anataka tatizo hilo liishe, hataki kijinga cha moto kwenye ndoa.)
IV. Mabadiliko ya Kiroho
A. Soma Hesabu 6:1-4. Kumbuka ya kwamba Mungu amewaweka Walawi wakfu. Ni fursa ipi hii inawapatia wale ambao hawakuzaliwa Walawi au wanaume? Je wale ambao hawakuzaliwa wakiwa walawi na wala si wanaume wanapata fursa gani hapa? (Hii inaonyesha kwamba hata katika kipindi cha Agano la Kale, Mungu alitamani kuwa na mahusiano maalum na mtu yeyote aliyekuwa tayari-bila kujali familia au jinsia.)
1. Unafikiri hii inahusianishwa na kanuni iliyotangulia? (Majaribu ya kingono yana nguvu sana . Mtu aliyetizama utaratibu uliotangulia angeweza kuamua kwamba anahitaji muda maalum na Mungu.)
2. Mungu anaelekeza kwamba mtu yeyote anayetaka kuwa na mahusiano maalum naye asiwe anakunywa pombe. Hiyo inahusianaje? (Ni mara ngapi dhambi ya uzinzi inahusisha pombe/ulevi?)
a. Panaonekana kuwepo na sababu dhahiri kwamba kwa nini kuwa mlevi ni kinyume na “nadhiri ya kujiweka wakfu kwa Bwana.” Lakini hii kanuni inakataza maji ya zabibu na hata zabibu kavu-kitu chochote kinachotokana na zabibu. Ni kwa jinsi gani ulaji wa zabibu kavu unaingilia mahusiano na Mungu?
3. Soma Mathayo 26:27-29. Yesu anasema nini kuhusu maisha yake ya baadaye na zabibu? (Kwamba hatakunywa tena hadi tutakapokutana naye mbinguni.)
4. Swali la vitendo: Ulaji wa zabibu na unywaji wa divai ulikuwa na nini hasa kwa watu waliokuwa janwani wakila mana pekee? Je, wote hawakuwa Wanazarayo (kwa kiwango flani) katika kipindi cha safari ya jangwani?
5. Unapokula kwenye sehemu ya kula vyakula vya Kimarekani (Taco Belt), Subway, McDonald au Burger King, je, unakunywa maji? (Si unakunywa soda? Kwa kawaida hizi sehemu zinauza vyakula vikavu pamoja na soda – Fadhili Ndimangwa kama hapo Bangalore huwa anaenda KFC Brigade Road kula kuku ni shahidi wa hili)
a. Vinywaji vyote vya aina ya soda katika sehemu hizi aidha vina caffeine au sukari au vyote. Sipendi kuwa na wasiwasi au kuwa mnene. Kuwa na wasiwasi na mnene ni kubaya sana ! Lakini,maji kwa ujumla yana ladha isiyo na mvuto. Hata kama yangekuwa yana ladha ya kuvutia, wengi wangependelea ladha ya kinywaji cha soda (soda kwa kawaida ina kaboni.))
6. Natumaini nimekufanya utafakari kwamba kwa nini divai ya zabibu inaonekana kuwa na tabia isiyo ya kawaida katika Biblia (na ninaamini hufikirii kuhusu vyakula vya fast food/madukani (vyakula kama vile chips, kuku wa kukaanga, pizza, burger, n.k. ambavyo ukifika tu unachukua na kuondoka au kula papohapo; ndio maana fast food nyingi zinaliwa pamoja na soda na sio mchuzi au supu, they are fast food, vya kula haraka haraka ukiwa safarini ama kwa hamu tu na sio kwenda kula kushiba ukiwa na njaa kali ama kula chakula bora). Kuna nini kuhusu divai ya zabibu (na mazao ya zabibu) ambacho ni maalum sana-ukilinganishwa na mahusiano maalum na Mungu? (Mara zote nimekuwa nikitafakari kuwa inahusisha kujikana nafsi. Jikane nafsi na utakuwa na mahusiano ya karibu na Mungu. Lakini, Frank Holbrook amenisaidia kutizama kwa undani zaidi. Alisema kwamba kupanda mizabibu ilionyesha kuwa umeweka makazi yako katika ardhi/nchi. Yesu “hajaweka makazi” hadi pale tutakapounganishwa naye tena. Hatupaswi kupiga kambi kwa mahusiano ya dhaifu na Mungu. Tunapaswa kuwa njiani kuelekea kwenye mahusiano bora na nyumbani kwetu pa milele!
V. Mibaraka ya Mwisho
A. Soma Hesabu 6:22-27. Rafiki, ungependa huu mbaraka? Unatoka kwa Mungu yule yule anayetupa maelekezo ya jinsi ya kuishi. Hebu fikiria hilo ? Mahusiano kati ya jinsi tunavyoishi na mibaraka ya Mungu!
VI. Juma lijalo: Ibada na Kujitoa wakfu
No comments:
Post a Comment