Friday, July 17, 2009

Somo la 4: Kutembea Nuruni: Kutunza Amri Zake

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N. Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk. Muombe Roho Mtakatifu akuongoze ujifunzapo somo hili.

 
 

Utangulizi: Mojawapo ya majukumu yangu kama mwanasheria ni kuthibitisha mada za kesi za wateja wangu. Ninapokuwa nikitetea kesi za kidini, kitu cha kwanza ni kuthibitisha kwamba mteja wangu ana "imani ya kidini ya dhati." Wewe ungefanyaje kuhusiana na hilo ? Utathibitishaje kwa hakimu, asiyemfahamu mteja wako, kile kilichomo moyoni mwa mteja wako? Ninatumia matendo ya mteja wangu kuthibitisha kile kilichomo moyoni mwake. Je, njia yangu ni njia ya Mungu? Matendo yetu yana uhusiano gani na kile kilichomo mioyoni mwetu? Hebu tujivinjari kwenye somo letu na kubaini kile ambacho Mungu anakisema kuhusu hili!


 

  1. Lengo
    1. Soma 1 Yohana 2:1. Wiki iliyopita tulijifunza kwamba wale "wanaotembea katika nuru" wana dhambi maishani mwao. (1 John 1:7-8) Je, hilo linakanusha matendo yangu = nadaharia ya moyo (heart theory)?
      1. Je, dhambi hiyo ni sawa tu kwa Yohana? Ni vipi kuhusiana na hilo kwa Mungu? Je, ni sahihi kutembea katika njia ya nuru ukiambatana na mzigo huu wa dhambi?
      2. Yohana anasema kuwa lengo ni nini? (1 Yohana 2:1: "Nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi." Lengo ni kuachana na dhambi.)
      3. Je, hili ni lengo halisi? Nini kinatokea endapo tutakosea? (Yohana anasema kuwa tunaye Yesu mtetezi wetu. Inafanana kabisa/Yesu anaonekana kama mwanasheria!)
    2. Angalia tena 1 Yohana 2:1. Yesu "anatuteteaje" mbele za Baba? Kwa kujenga hoja kwamba kila mtu anatenda dhambi, na kwamba Mungu asiangalie dhambi mojamoja?
      1. Je, Yesu anajenga hoja kwamba kile tulichokifanya hakikuwa dhambi haswa?
    3. Soma 1 Yohana 1:10. Ni watu wa aina gani tulioamua wiki iliyopita kuwa ndio walioelezewa hapa? (Haya ni makundi mawili: Kwanza, wale wanaodai kuwa wamefikia kiwango cha ukamilifu na kwamba hawana dhambi. Pili, wale wanaosema kuwa hawatendi dhambi sasa na kamwe hawajawahi kutenda dhambi kwa sababu dhambi kwa hakika haipo kwa ajili ya Wakristo. Inaleta mantiki kwamba Yesu asingekuwa anarudia kubadilika kwa hizi hoja mbili potofu.)
    4. Unafikiri watu walioelezewa katika 1 Yohana 1:10 ndio wale wale ambao Yohana anazungumza nao katika 1 Yohana 2:1? (Hapana. Yohana anaanza kwa kusema "watoto wangu wadogo." Haendelei kuzungumza na kundi la watu wale wale aliokuwa akiwaongelea katika fungu la 10. Alisema kuwa watu walioelezewa kwenye fungu la 10 walikuwa wanamfanya Mungu kuwa mwongo na neno la Mungu halina nafasi maishani mwao. Yohana amegeukia kundi lingine la watu wanaoutafuta ukweli. Hawa ni watu wanaotembea kwenye njia
      ya nuru. Hawa ni watu wanaotaka mioyo yao na matendo yao kushabihiana/kuendana.)

    5. Sasa kwamba tumeshajadili kile tunachofikiri Yesu anaweza kukijengea hoja, hebu tusome 1 Yohana 2:2 na kujaribu kuona kama tunaweza kubaini kile ambacho kwa hakika anakijengea hoja. Ni hoja ya aina gani inapendekezwa ambayo Yesu anaifanya badala yetu?
      1. Fikiria kwamba umeburuzwa mbele ya hakimu na unashitakiwa kwa kufanya kosa la jinai. Na pindi usimamapo na kujaribu kujiweka vizuri (na kutokuwa kwako na hatia) mara unamsikia wakili wako akianza kujenga hoja zake: "Mheshimiwa, mteja wangu ana hatia, tena ana hatia sana….." Ungesema nini?
        1. Je, huo ndio utetezi wa Yesu kwa ajili yetu? (Ndiyo! Utetezi wake ni kwamba tuna hatia sana , lakini tayari amekwishalipa adhabu. Habishani dhidi ya hatia yetu. Anabisha dhidi ya adhabu nayowekwa juu yetu.)
      2. Katika muktadha wa hoja ya Yesu (wakili wako), ni vipi juhudi zetu za kuficha na kukataa dhambi zetu zinaonekana? Fikiria hatua ya hakimu kama ungeanza kupingana na wakili wako na kauli ya kuudhi, "Sina hatia! Naishi maisha makamilifu! Matatizo yoyote ninayoweza kuwa nayo siwajibiki nayo. Ni makosa ya kurithi niliyoyapata kutoka kwa baba yangu na mama yangu!"
    6. Tumeamua dakika chache zilizopita kuwa 1 Yohana 2:1 imeelekezwa kwa "wale walio katika njia yenye nuru." Je,hili liko sawa na 1 Yohana 2:2? (Kafara ya Yesu ni "kwa ajili ya dhambi za dunia yote." Kafara yake inaweza isikubaliwe na wote, lakini aliyatoa maisha yake kwa kila mtu.)
    7. Fikiria hili: Kwa nini Yohana anamuwianisha Yesu kama anayetutetea au anayepigania nafsi yetu kwa Mungu? Je, Mungu Baba anahitaji kushawishiwa? Je, hii ni aina fulani ya mjadala ambayo tunatumai kuwa Yesu anashinda?
    8. Soma Yohana 16:26-27 ambapo Yesu anasema kuwa "wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda….." Hili linalinganaje na uhitaji wa wakili? (Utetezi wa Yesu ni kinyume na matakwa ya sheria, na siyo matakwa ya uhasama (kwetu, badala ya juu ya dhambi) ya Baba. Kile ambacho Yesu ametutendea ni zaidi ya maneno ya kuelezeka, na ukweli kwamba Yesu anajitokeza mbele kwa niaba yetu hufanya utetezi wetu kuwa dhahiri.
  2. Kumjua Mungu
    1. Soma 1 Yohana 2:3-4. Mara kwa mara mtu fulani huniuliza kama namfahamu mtu fulani muhimu. (Kwa kweli, kwa ujumla huwa ni kinyume,huwa nina shauku kuwaelezea wengine kama namfahamu mtu yeyote ambaye si wa muhimu. Ina maanisha nini "kumjua" mtu fulani? Yohana anamaanisha nini anapotuandikia sisi kuwa anamjua Yesu? (Kumjua mtu fulani inamaanisha kuwa unafahamu kitu fulani kumhusu.)
      1. Kama hili ni kweli, sasa kwa nini tena utii wa sheria ya Mungu ni "kipimo cha uhalisia" wa kumjua Mungu? (Kimantiki, lazima imaanishe kuwa kuna muunganiko thabiti kati ya kumjua Yesu na kujua amri zake.)
      2. Je, hili linathibitisha mtazamo wangu wa kimahakama: kwamba matendo ya mteja wangu yanaelekea kuonyesha endapo mteja "anamjua" Yesu? Ana moyo kwa ajili ya Yesu?
    2. Kwa nini Yohana anasema kuwa tumheshimu Yesu?  Motisha yetu ni nini? (Tunamjua.)
      1. Kwa nini Yohana hasemi tutii kwa sababu tunajua kanuni?
      2. Kwa Yohana hasemi  tutii kwa sababu tunamcha Mungu?
      3. Kwa nini Yohana hasemi  tutii kwa sababu tumepitia uzoefu wa changamoto ngumu kabisa ama uzoefu wa raha na hali njema
    3. Je, hii ni kanuni ya Ulimwengu? Ya kwamba tutii kile tunachokijua?
      1. Kama utasema, "ndiyo," jiulize kuwa ulitumia muda gani kumjua Mungu wiki iliyopita ukilinganisha na kulijua joka likiongea kupitia kwenye televisheni?  
    4. Kama utasema, "siyo kweli, Bruce, kwamba natii kila kitu ninachokijua," basi kwa nini kumjua Mungu inamaanisha kuwa tumtii? (Hii inasema chemsha bongo fulani kuhusu Mungu. Pendo lake na tabia yake ni kwamba kumjua hutufanya tutake kutii!)
    5. Marafiki zangu, hili ni jambo linaloua: hatuwezi kumtii Mungu isipokuwa kama tunamjua. Upande mwingine wa mlinganyo huu ni makini zaidi: hatumjui kama hatumtii.)
    6. Soma 1 Yohana 2:5. Unafikiri Yohana anamaanisha nini pale anaposema kuwa upendo wa Mungu umekamilika kwa yeyote yule anayetii? (Ukristo siyo wa kinadharia. Siyo uelewa wa kanuni  zinazodhanika ambazo hazileti utofauti wa kivitendo katika maisha yetu. Upendo wa Mungu unakamilika kwetu pale tunaporuhusu mapenzi yake yabadilishe matendo yetu.)
    7. Soma 1 Yohana 2:6. Inamaanisha nini "kutembea" kama Yesu alivyoenenda? Je, inamaanisha kuwa:
      1. Hatuna fedha?
      2. Hatuna mke/mume (mwenza)?
      3. Tunahubiri? (Yohana kwa hakika, kwa uwiano sahihi, anaelekeza dhana kuwa utii ni wa msingi sana . Haongelei kuhusu masuala fulani ya maisha ya Yesu, anaongelea kuhusu dhamira ya Yesu ya kumtii Baba yake na kuakisi mapenzi ya Baba yake. Mioyo yetu na matendo yetu ina uhusiano.)
  3. Matokeo ya Kumjua Mungu.
    1. Soma 1 Yohana 2:7-8. Je, Yohana anatukumbushia kuhusu amri ya zamani au anatuambia kuhusu amri mpya? Yohana anaanza kwa kile kinachoonekana kama vile ana kipingamizi: "siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani. Labda ni aina fulani ya amri mpya." Ni ipi hii? (Ni amri ya zamani ambayo haitambuliki kwa dhahiri hapo kabla kwa sababu mwanga mpya unaturuhusu kuiona.)
      1. Umewahi kupata kitu cha kale, ukakisafisha, na kudhani kuwa kimeonekana tofauti kabisa? Kipya kabisa?
    2. Soma 1 Yohana 2:9-11. Je, hii sheria ya kale iliyofanywa kuwa mpya ni ipi? (Kuwapenda Wakristo wenzetu).
      1. Imewezwaje kufanywa upya? Asili ya mwanga mpya ni ipi? (Hujui namna ya kupenda, Yohana anasema, hadi mmeona jinsi Yesu alivyopenda! Yesu "alisafisha" upendo wa kale na dhana/wazo la utii kutupatia mfano wa kile kilichodhamiriwa. Chukulia mifano miwili: 1) Mkono uliopooza uliponywa siku ya Sabato (Mathayo 12); na, 2) Mjadala wa Yesu kuhusu umuhimu wa kile kitokacho kinywani badala ya kile kiingiacho kinywani (Mathayo 15).)
    3. Rafiki, unapima vipi uhalisia wa 1 Yohana 2:9-11? Matendo yako yanasema nini kuhusu moyo wako? Je, unamchukia mtu yeyote? Una vinyongo na watu? Mtizamo wako ni upi kwa familia ya Mungu? Jibu la maswali haya linaonyesha kama upo kwenye njia yenye "nuru" au njia yenye " giza ".

 
 

  1. Wiki Ijayo: Kutembea Nuruni: Kuyakana Mambo ya Ulimwengu.


 

No comments:

Post a Comment