Monday, July 6, 2009

SOMO LA 2: KUPATA UZOEFU WA NENO LA MUNGU

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2009, Bruce N.Cameron, J.D. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sememu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Somo hili pia linaweza kupatikana kutoka kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kizulu, nk.

Utangulizi: Nipo Kalifornia kwa sasa. Kwa miaka mingi niliyokuwa nikitembelea Kalifornia nimejifunza kwamba sehemu kubwa ya wakazi wake hupenda kuonekana wadogo. Kundi hili linakinzana na mfumo wa asili wa maisha ambapo umri mkubwa hutamaniwa kwa kuwahuleta busara na heshima. Badala yake, kila mtu hutaka kuonekana mdogo milele. Kwa nini iko hivi? Nafikiri sehemu kubwa ya sababu ni kuwa ujana ni sawa na maisha yenye msisimko. Utu uzima wenyewe nao ni sawa na kifo. Ujana na maisha ni mambo ya kusisimua na yenye mvuto. Kifo kwa kweli chenyewe huchukiza. Somo letu wiki hii linapendekeza njia nyingine ya maisha (na ujana. Je wewe ni mtu atakaye kuwa kijana milele? Unatamani furaha ya maisha? Basi na tuzame katiaka somo letu na tuona zaidi juu ya maisha ya milele na ujana.

I. Shuhuda wa Maisha

A. Tusome 1 Yohana 1:2. Wiki iliyopita tulijadili kauli ya Yohana ya kwamba Yesu ni “neno” la uzima. Sasa Yohana anasisitiza sehemu ya pili ya sentensi “uzima.” Ni nini kilicho muhimu katika kumuita Yesu “Uzima” wakati tayari tumeshamwita “Neno?”

1. Je umewahi kusikia mtu akizungumzia mada na ukahitimisha ya kuwa hawafahamu wanachozungumzia? (Yohana anatuambia ya kwamaba Yesu siyo tu kwamba anatupa maelekezo kuhusu maisha (“Neno”), bali Yesu ni uzima.)

2. Ni kwa jinsi gani Yesu ni “Uzima?” (Wiki iliyopita tulijifunza kwamba Yesu ni muumba wetu, hii humfanya yeye kuwa asili ya uzima. Yohana anashuhudia ya kwamba Yesu alifufuka nay a kwamba yu hai. Hii inaonyesha kwamba Yesu anao uzima sasa. Ufufuo unaonyesha nguvu ya “uzima” hata katika nyakati ambapo kifo kimetokea.

B. Wakati Yohana akiandika katika 1 Yohana 1:2 kwamaba “uzima huo ulipodhihirika” ni hoja gani anayojaribu kuijenga? Mara mbili ametumia neno “kudhihirika.” Je ungeweza kusema (juu ya mtu mwingine) ya kwamba “wanadhihirika” (Hapana. Mungu hudhihirika kwa wanadamu. Yohana anatuambia kwamba Mungu alifanyika mwili na kasha Mungu akaungana na wanadamu wengine. “Uhai huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu..” Kiini ni katika Mungu kushuka chini na kudhihirika kwa wanadamu.)

1. Je Yohana anafundidha nini juu ya uhusiano wa Yesu na Baba Mbinguni? (Yohana hajengi utata katika hili. Anasema kwamba Yesu alikuwa na Mungu na kisha akatokea kama mwanadamu. Yesu alikuwa na asili yake mbinguni. Aidha uliamini hili au usiliamini. Hauwezi tu kwa mantiki, kama baadhi ya viongozi wa kidini na watu wengine, uamini ya kwamba Yesu alikuwa tu ni rabbi mwenye busara au mtu mzuri.kufanya hivyo kunamfanya Yesu na wale wote waliokuwa wasshriki wake kuwa ni waongo wenye kufedhehesha. Aidha ukubali imani itawale au ukatae. Hakuna msimamo wa kati katika hili.)

C. Soma 1 Yohana 1:3. Je ni kauli gani nyingine tena aletayo Yohana juuu ya Yesu? (Anatuambia ya kwamba mbali na asili ya Yesu kuwa mbinguni, Yesu ni “Mwana” wa Mungu. Anatoa taswira ya ulimwengu kwa kuita sehemu moja kuwa “Father” na nyingine “Mwana”)

1. Hii si mada ya juujuu. Soma Kumb. 6:4. Hili lilikuwa mojawapo ya fungu la muhimu sana kwenye Biblia kwa mujibu wa wachambuzi wa kiyahudi wa nyakati za Yohana. Tunatatuaje hili jambo na taswira ya Yesu kuwa mwana wa Mungu? Yesu anawezaje kuwa Mungu, wakati kuna Mungu mmoja tu?

a. Tafakari kidogo katika fungu hili la Kumb 6:4. Utawezaje andika hili isipokuwa Mungu wako ana Nyanja? (Nafikiri hii inasisitiza dhana ya Utatu, wazo ya kwamba Yesu na Mungu Baba ni Mungu mmoja.)

2. Soma Mwanzo 1:1-2. Neno la kkiebrania “Mungu” katiak aya ya kwanza ni neno la wingi. Je hii hutufundisja nini juu ya Utattu? (Katika injili yake na nyaraka zake Yohana anaanza uandika kama kitabu cha Mwanzo. Ni katika kitabu cha Mwanzo tunaona dhana ya Mungu kuonyesha Utatu. Yohana anaelezea ya kwamba utatu huu unamjumuisha Yesu kama Mwana na Muumba.)

II. Shuhuda wa Upendo

A. Tazama tena katika 1 Yohana 1:3. Ni kwanini Yohana anasema anatoa ushuhuda wake juu ya Yesu? Ni nini nia yake? (ili wasomaji wake wa waweze kuwa na shirika naye.)

1. Yohana ameshafariki. Twataabikia nini? Ni aina gani ya shirika aliyo nayo Yohana? (Yohana anasema ushirika wake hakika ni wa pekee. Yohana anafanya shirika na “Ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na mwana wake Yesu kristo.)

B. Zingatia yaliyomo katika ushuhuda wa Yohana katika 1 Yohana 1:3. Anaunganisha “ushirika” na kile alichokiona na kukisikia. Ni kwa jinsi gani hiyo inatusaidia kuwa na shirika na Mungu Baba na Mungu Mwana, Yesu? (Kama tusipoelewa asili ya Mungu na ya kwamba Yesu ni Mungu, hatuwezi kuwa na shirika na Mungu.)

1. Hata hivyo, kuwa na shirika ni nini, hata tutamani hivyo? (Kuwa shirika ni kumfahamu mtu, kuwa na muda naye wa pamoja. Yohana anasema, “tazama nimekuwa na muda na Yesu. Namfahamu. Endapo kama utatumia muda wako na ujumbe huu, utakuwa “unatumia muda” wako ukiwa na Yesu na utamfahamu.”)

a. Je unafurahia kusoma kitabu hiki? Kuwa na fursa ya kumjua Yesu na kuwa na shirika na Mungu?

C. Soma Yohana 14:7-9. Yesu anasema kuwa tukimjua yeye, tumemju aBaba. Je Yohana anaelezea zaidi kauli ya Yesu? (Yesu ni Mungu na shahidi wa mambo ya mbinguni. Yohana ni shahidi wa Yesu. Tuna mtiririko wa kuaminika wa taarifa.

D. Soma 1 Yohana 1:4. Je kauli hii si kwamba ingesema ya kwamba Yohana anatuandikia ili kutimiza furaha yetu badala ya kutimiza na furaha yake pia? Hata hivyo, yeye tayari anamjua Yesu. Yeye tayari yupo kwenye hili kundi malum lenye shirika na Yesu.

1. Hebu fikiria mtu akwambie kwamba atakupeleka ikulu ya Marekani (tena pasi gharama) na kukutambulisha kwa rais wa Marekani. Je haitokuwa bayana ya kwamba lengo lilikuwa kufanya siku yako kuwa njema badala ya kufanya siku ya mheshimiwa rais njema?

2. Hebu jenga picha ya taswira na fikiria ya kwamba umepelekwa kwenye klabu ya Muumba na Bwana wa ulimwengu. Je hi ni kwa manufaa yako au yake?

3. Ni kwanini Yohana ana mtizamo huu wenye kuonekana kinyume? (Kitu kisicho cha kawaida na muhimu sana kinasemwa hapa: Mungu anataka ushirika na wewe. Inampa Mungu furaha kuwa na shirika na sisi!)

E. Soma Yohana 15:15. Ni uhusiano wa aina gani ambao Mungu anataka kuwa nao nasi? Je ni wazo gani yeye mwenye uzima wa milele analo juu yetu? ( Yesu anatuita sisi “rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.” Fungu linalofuata linaendelea kwa kusema kwamba Yesu alituchagua sisi, hatukumchagua yeye. Alitutaka sisi ali tuweze kuwa naye kwake!)

1. Je huleta hisia gani kuwa rafiki wa Mungu?
2. Je waweza tumia furaha zaidi katika maisha yako?
3. Dhambi ina raha zake, ama la hakuna ambaye angafanya dhambi. Kama una uzoefu na dhambi nzito, je waweza shuhudia ya kwamba utii kwa Mungu huleta furaha halisi na ya kudumu?

a. Hebu fikiria uzoefu wa Gavana wa Kalifornia Kusini (ambaye majuzi alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa wa muda mrefu). Kama angekuwa na fursa ya kuandika tena historia yake katika kiaka michache iliyopita, je unafikiri angefanya nini? (Kwa wasomaji wasiofahamu Gavana amefedheheshwa sana, angeweza kupoteza familia yake na amepoteza sifa ya kuwa makamu wa rais wa Marekani kwa sababu alijihusisha na uhusuano wa kimapenzi na mwanamke mmoja wa Argentina.) Je, unafikiri ana furaha sasa?

F. Katika 1 Yohana 1:4 Yohana anajijumuisha katika “furaha yetu.” Pale tuletapo wengine katika kundi hili la wenye urafiki na Mungu, je huleta furaha?

G. Rafiki ungependa kuwa rafiki wa Mungu? Je, ungependa kuingia katika jamii yenye nguvu kabisa ya mawiliki katika ulimwengu? Ungependa furaha ya kudumu? Kama ndivyo, wiki ijayo na tuedelee na safari yetu ya kusoma na kujifunza zaidi juu ya ujumbe wa Yohana kwetu.

III. Wiki ijayo: Kutembea Nuruni: Kugeuka na Kuiacha Dhambi

No comments:

Post a Comment