Monday, February 15, 2010

THISDASO ASSOCIATES WATEMBELEA HOSPITALI YA KISARAWE

Vijana waliokuwa wanachama wa chama cha wanafunzi wa Kisabato katika vyuo walifanya huduma ya kwenda kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Kisarawe iliyopo mkoa wa pwani. Katika programu hiyo iliyoitwa "Huduma yangu kwa Yesu" zaidi ya watu thelathini na mbili (32) walishiriki. Huduma hiyo ilianza kwa wana na binti za Mungu kusali na kupata fursa ya kuhudumu katika kanisa la Kisarawe na ndipo mchana wakaenda hospitali.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo


Wakati wa mjadala wa lesoni kanisa la wasabato Kisarawe


Maandalizi kwa ajili ya huduma kuu, kutoka kulia, Enos Manusu, James Sanawa, Rubara Marando na Bambino Philips


Muimbishaji, Nelson Nyahonyo akiongoza wimbo wakati wa huduma kuu


Kikundi cha uimbaji cha ZION MELODY kikiimba wakati wa ibada


Kusabahiana baada ya huduma


Kusabahiana kwa kukumbatiana miongoni mwa wasafiri wa mbinguni


Wana ASSA na wana THISDASO wa zamani wakiwa pamoja


Kutangaziwa utaratibu mzima utakaofuata kuelekea "huduma yangu kwa Yesu"


Kabla ya kwenda hospitali thisdas_sociates walikabidhi vitu kwa ajili ya kapu la DORCAS baada ya ibada


Muda wa kuhudumia hekalu la Bwana


Watu wa Mungu wakitumia


Watumishi wakipanga vitu kupeleka kwa wasioweza katika hospitali ya Kisarawe


Watumishi hawakutoa vinyonge bali walijinyima kwa ajili ya ndugu zao




Wajoli wakiingia wodini tayari kuwatendea miongoni mwa wale walio wadogo


Mgonjwa akifarijiwa na dada Neema Opiyo


Mrs. Tang'are aitwaye Jessie na Naphtali wakiwapa faraja wagonjwa


Katika kila wodi baada ya kuongea na wagonjwa na kuwapa faraja basi tulipata muda wa kuwaombea.


Heart to heart (this is my favorite picture)


Daktari mkuu Mr. Ogha akiongea na wageni kuwashukuru kwa huduma yao ya kuwatembelea


Viongozi wa kamati yetu ya programu kuanzia kushoto ni mwenyekiti ndugu Enos Manusu na ndugu Bambino Philip


Kijana Eliya wa Minaki akiaga kwa niaba ya wenzake baada ya huduma


Kundi zima la waliohudumu siku hiyo wana thisdas_sociates, isipokuwa Mgune Masatu (mpiga picha,)washiriki wa kanisa la Kisarawe,Mganga mkuu na wana ASSA wa Minaki sekondari.


Mpiga picha wetu ndugu Mgune Masatu

Shukrani kwa wana thisdas_sociates kwa kuandaa tukio hilo zuri kwa watu wa Bwana kwenda kutoa huduma katika jamii, shukrani pia kwa mzee wa kanisa la Kisarawe mzee Clauds na kanisa zima kwa ujumla kwa kutupa ushirikiano katika uendeshaji wa zoezi zima, shukrani kwa mamlaka za hospitali zilizotufungulia mikono na kutuwezesha kuwafikia wenzetu,shukrni kwa wanafunzi wa MInaki sekondari, shukrani pia kwa mtu mmojammoja ambaye alijikana nafsi kwa namna moja ama nyingine ili kuliinua jina la Bwana na mwisho shukrani kwa Mungu wetu wa mbinguni aliye mmiliki wa vyote na aliyetupa vyote tuvitumie kwa utukufu wake. Bwana atubariki tunavyozidi kutafakari kuwatendea miongoni mwa wale walio wadogo.